Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Maulavi Muhammad Amjad Khan, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu Pakistan, katika hotuba yake kuhusiana na hali ya Ghaza na mauwaji ya kimbari yanayo endelea katika eneo hilo, sambamba na kulaani jinai zinazofanywa na Israel pamoja na ushirikiano wa baadhi ya nguvu za kibeberu duniani, alisisitiza juu ya ushujaa na uimara wa watu wa Ghaza.
Akiendelea na hotuba yake huku akigusia dhulma na ukatili ulio kithiri, alisema: Dhulma inayo endelea kwenye ukanda wa Ghaza imekuwa ni ya hali ya juu sana; maiti nyingi zimejaa mitaani na mito ya damu inatiririka, lakini dhamira ya dunia imelala, hata hivyo, watu wa Ghaza kwa ushujaa wa kipekee wamesimama imara mbele ya jinai na ugaidi wa Israel na wakavuruga njama za maadui.
Maulavi Amjad Khan aliongeza kwa kusema: Marekani na Israel walikusudia kwa kuharibu majengo na kuleta maangamizi kuthibitisha ubabe wao, lakini kamwe hawatafanikiwa.
Akiashiria ukatili wa adui, alibainisha kuwa: Hata watoto waliokuwa wamesimama foleni ili kupata chakula hawakunusurika na risasi, hata hivyo watu wapenda uhuru na mujahidina wa Ghaza bado wapo katika uwanja wa mapambano.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu Pakistan alitathmini nafasi ya Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na migogoro ya kibinadamu kuwa ni sifuri, na akaongeza kusema: Kwa masikitiko nchi nyingi za Kiislamu pia hazikuonyesha ushujaa unaohitajika, lakini licha ya mashinikizo yote na ukatili, kushindwa kwa Israel na kufeli kwake ni jambo la hakika.
Maoni yako