Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, shughuli hii adhimu ya pili ya Siku ya Hussein (a.s) iliandaliwa na mtandao wa Kimataifa wa Khayrul-ʿAmal katika Bunge la Jimbo la Victoria, Australia, tukio hili la kiroho na la kipekee liliudhuriwa na idadi ya wawakilishi wa bunge, viongozi wa vyuo na taasisi za kielimu, pamoja na viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali kama vile Shia, Sunni, Wakristo, Wahindu na Wasikh, Washiriki wote kwa mshikamano na heshima walitukuza ujumbe wa haki, uhuru na ubinadamu wa Imamu Hussein (a.s).
Hafla hii ilianza chini ya usimamizi na uongozi wa Sayyid Asad Taqavi, Mwenyekiti wa Mtandao wa Khayrul-ʿAmal, Katika hotuba yake ya awali, baada ya kuwakaribisha wageni, alisisitiza juu ya umuhimu wa kufikisha ujumbe wa Hussein kwenye jamii ya kimataifa, na akatoa mtazamo wa kuandaliwa programu kama hizi na kuwa ni hatua yenye thamani kubwa katika kuutambulisha utamaduni wa Ashura kwenye ngazi ya kimataifa.
Baada ya hapo, ujumbe wa sauti wa Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Sayyid Abulqāsim Ridawi, Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Australia na Imamu wa Ijumaa wa Melbourne, ambao ulitumwa kutoka karibu na Haram Tukufu ya Imamu Hussein (a.s), ulisikilizwa.
Katika ujumbe wake, huku akigusia kudumu kwa mapinduzi ya Ashura, alisema: “Imamu Hussein (a.s) alifikisha ujumbe wa heshima kwa mwanadamu, haki na maadili, kikao cha leo cha wawakilishi wa dini na jamii mbalimbali katika Bunge la Australia ni ushahidi bora wa ujumbe huu kuwa wa kimataifa, pamoja na kuwa sipo pamoja nanyi huko, lakini najiona kuwa mwakilishi wenu nyote katika ardhi hii tukufu, Na uhusiano huu kati ya Karbala na Bunge la Australia ni alama dhahiri ya upeo na kina cha ujumbe wa Hussein (a.s).”
Picha ikionesha muendelezo wa kikao hicho
Kisha Hujjatul-Islam Sayyid Muhammad ʿAli ʿAwn Naqawi, mjumbe wa baraza la kielimu la Jāmiʿat al-Mustafā al-ʿĀlamiyya, kama mgeni rasmi, alitoa hotuba yake ya kwanza ndani ya Bunge la Australia, akiashiria jinsi harakati ya Ashura ilivyokuwa ni ya kilimwengu, alisema: “Leo ndani ya moyo wa bunge la nchi ya Magharibi, sauti ya kudai haki ya Imamu Hussein (a.s) inasikika, na hii ni alama iliyo wazi ya kudumu ujumbe wake, Katika zama hizi ambapo dunia imezongwa na dhulma, ukatili na ukosefu wa haki, kuliko wakati mwingine wowote tunahitajia kuueneza na kuutangaza ujumbe wa Hussein (a.s).”
Katika mwendelezo wa hafla hiyo, viongozi kadhaa wa kidini na kijamii wakiwemo viongozi wa dini ya Kihindu na Usikh, pamoja na baadhi ya wawakilishi wa bunge, walitoa hotuba zo huku wakiheshimu nafasi tukufu ya Imamu Hussein (a.s), walisistiza juu ya nafasi yake kwenye kutoa msukumo katika kueneza amani, usawa, haki na kuishi kwa mshikamano kati ya mataifa na dini.
Zaidi ya hayo, baadhi ya wajumbe wa Baraza la Maulamaa wa Kishia walihudhuria mkutano huu, na sambamba na kusisitiza umuhimu wa kufanyika kwa matukio kama haya, walibainisha haja ya kuendelea kuitambulisha dunia ujumbe wa Ashura katika majukwaa ya kimataifa.
Sherehe ya Siku ya Hussein (a.s) katika Bunge la Victoria ilikuwa ni taswira iliyo wazi ya mshikamano wa dini na tamaduni mbalimbali; tukio lililodhihirisha kuwa ujumbe wa Ashura uko juu ya mipaka ya kijiografia, kidini na kikabila, mkutano huu haukukumbusha tu kujitolea na kujitoa muhanga kwa Imamu Hussein (a.s), bali pia uliandaa mazingira yenye thamani ya kukuza thamani za kibinadamu, haki ya kijamii na kuishi kwa amani duniani kote.
Maoni yako