Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Taasisi ya Hujjatul Asr Society of Tanzania chini ya usimamizi wa Sayyd Arifu Naqawi imefanikisha kwa ufanisi mkubwa maadhimisho ya Arubaini ya Imam Husseini (as) kwenye vituo vyake mbalimbali vilivyopo nchini Tanzania.
Katika maadhimisho hayo shughuli mbali mbali ziliripotiwa kufanyika, shughuli ambazo zilijumuisha watu kutoka maeneo mbali mbali, miongoni mwa shughuli zilizo fanikishwa na Taasisis hiyo ni kama zifuatazo:
Mosi, majlisi za huzuni zilizokuwa zimebeba ujumbe mzima wa historia ya Karbala ambayo inamuhusu Imam Hussein na maswahaba wake walio uwawa kidhalimu katika ardhi hiyo, huku majlisi hizo zikihusishwa na kujenga mazingatio ya kiroho.
Pili, Maatam na Nawha mbalimbali ambazo zilisomwa huku waumini wakionesha mapenzi na masikitiko yao juu ya Ahlulbayt (as) kupitia nawha hizo.
Tatu, swala ya Jamaa Iliyoongozwa na Sayyid A'rif, swala ambayo ilikuwa ni alama thabiti iliyolenga kuonesha umoja na mshikamano kwa waumini wote walio fanikiwa kuhudhuria, huku ikiwa na ujumbe ulio ashiria umuhimu wa ibada ya pamoja.
Maadhimisho haya yameacha athari kubwa kwa waumini kwa kuwa yameongeza mapenzi na utiifu juu ya Ahlulbayt (as), na yameimarisha umoja na mshikamano katika kijamii iliyo wazunguka, hata hivyo Taasisi ya Hujjatul Asr Society of Tanzania inaendelea kujitolea katika kuzienzi kumbukumbu hizi muhimu kwa ajili ya malezi ya kiroho katika jamii waliyo ambatana nayo.
Baadhi ya picha mbali mbali zikionesha ushiriki wa waumini kwenye hafla hiyo
Maoni yako