Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Zainul Abidin, mtafiti na mhubiri kutoka India, katika mazungumzo maalum na mwandishi wa habari wa Hawzah, amesisitiza nafasi ya sira ya Mtume Muhammad (saw) na Imam Hasan (as), akasema: Sira hii imejaa mafundisho ya uongozi na siasa na inaweza kuwa mfano wa kudumu na mwongozo kwa viongozi na wanasiasa wa leo.
Muendelezo wa mahojiano haya ni kama ifuatavyo:
Swali
Je! Ni vipi uongozi wa Mtume (saw) na Imam Hasan (as) utaweza kutumika katika mazingira ya sasa?
Jibu
Hujjatul-Islam Zainul Abidin: Sira ya wateule hawa imejaa mafundisho ya uongozi na siasa, uongozi wao ulikuwa ukitokana na haki, uaminifu, subira na uvumilivu, na misingi hii inaweza kuwa taa ya mwongozo kwa wanasiasa wa leo.
Swali
Ikiwa tungehitaji kuonyesha sifa muhimu za uongozi wa kidini, ni nukta zipi unazozipendekeza?
Jibu
Sifa ya kwanza ni uaminifu na haki, Mtume (saw) alionyesha kuwa madaraka si chombo cha unyanyasaji, bali jukumu la kulinda wanyonge na kupigania na kupinga ufisadi.
Sifa ya pili ni subira na uvumilivu; Imam Hasan (as) alichagua amani na diplomasia badala ya vita visivyo na matokeo mbele ya shinikizo na adui wa wakati wake. Sifa ya tatu ni uhifadhi wa umoja wa taifa, historia imethibitisha kuwa heshima ya pande zote na mshikamano wa kijamii ni siri ya mafanikio ya taifa lolote.
Swali
Kwa kuzingatia sifa hizi, je wanasiasa wa leo wameweza kutumia mafundisho haya?
Jawabu
Kwa bahati mbaya, mara nyingi maslahi ya kisiasa huzidi thamani za Kiungu, jambo linalosababisha kutofuata mafundisho haya, hata hivyo, wananchi pia wana jukumu la kuomba uongozi mzuri na waaminifu kutoka kwa viongozi na kuzingatia uaminifu na haki katika uchaguzi wao.
Swali
Ni nafasi gani jamii na hasa vijana wanapaswa kuchukua katika kutimiza mafundisho haya?
Jawabu
Jamii inapaswa kushikamana na ukweli na haki, vijana kwa kupata elimu sahihi na kuelewa historia ya Uislamu wanaweza kuelewa wajibu wao wa kisiasa na kijamii, ikiwa uelewa huu utaenea kati ya vizazi vijavyo, viongozi hawatakuwa na budi bali lazima wafuate maadili.
Swali
Mwisho, ni hatua gani unazozipendekeza zitumike ili kuingiza mafundisho haya katika jamii?
Jawabu
Kwanza, historia ya Uislamu na maadili ya kisiasa inapaswa kupewa kipaumbele katika mfumo wa elimu, vyombo vya habari na taasisi za kidini pia vina jukumu la kuuelimisha umma, zaidi ya yote, lazima tuifanye sira ya Mtume (saw) na Imam Hasan (as) kama sehemu ya maisha yetu ya kila siku, iwe kwa vitendo vya pamoja na mtu binafsi, ndipo jamii yenye haki, mshikamano na maendeleo itakayoundwa.
Maoni yako