Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, kutoka Rasht, Ustadh Reza Ramadhanii, mwakilishi wa watu wa Gilan katika Baraza la Wanazuoni Wateule wa Kiongozi wa Mapinduzi (Majlis khobregani), usiku wa Jumapili tarehe 8 Tir, katika maombolezo ya siku ya tatu ya Muharram yaliyofanyika katika Haram ya Sayyidah Fatimah al-Ukhrā (as) mjini Rasht, alisisitiza juu ya ulazima wa kuyabadilisha maombolezo ya Muharram kuwa majukwaa ya “harakati za vitendo”. Alionya na kuongeza kuwa: Kuhisi huzuni na majonzi kwa kiwango cha hisia tu bila kuingia kwenye uwanja wa kutetea haki, kunapelekea kupotoshwa kwa tukio la Karbala. Iran ya leo ni “shule ya kulea kizazi cha ‘Ashura,” na bendera ya mapambano dhidi ya dhulma imo mikononi mwa Kiongozi wa Mapinduzi.
Ramadhanii, kwa kurejea mwenendo wa baadhi ya watu katika tukio la Karbala, alisema: Wengi walikimbia uwanja wa mapambano kwa sababu ya woga, na hata baadhi yao walipotosha simulizi ya Karbala. Uwasilishaji wa uongo wa masaibu ya Ahlul-Bayt (as) bado ni tishio kubwa hadi leo, na vituo vya maombolezo vinapaswa kuzuia upotoshaji kwa kuwasilisha ukweli kwa usahihi.
Mwakilishi huyu wa Baraza la Wanazuoni Wateule aligusia jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni, na kusisitiza kuwa: Mashujaa wetu mashahidi walikuwa ni watangazaji wa Ghadir na ‘Ashura, na walisimama dhidi ya utumwa na ubaguzi wa kikabila wa maadui. Madhehebu ya Imam Hussein (as) hayakubali fedheha, na leo hii bendera ya Ghadir ipo mikononi mwa Imam Khamenei, ikiwa ni alama ya kupambana na mabeberu wa kimataifa.
Umuhimu wa kubadili machozi kuwa vitendo
Ramadhani alieleza kuwa, kulia katika maombolezo kunakuwa na thamani pale tu kunapopelekea "marekebisho katika jamii, kusimama dhidi ya dhalimu, na kuleta uadilifu." Aliongeza kuwa: Kuelewa ukweli wa masaibu humgeuza mtu kuwa mtekelezaji na mwenye kuhusika. Iwapo kikao cha Imam Hussein (as) hakikushughulikia matatizo ya sasa ya Uislamu na masaibu ya Maimamu, basi kimepuuza uwezo wake kamili.
Akiwakumbusha watu kuhusu shakhsia kama Ayatollah Modarres, Imam Khomeini (ra) na mashahidi wa Mapinduzi, alisema: Wote hao walikumbana na matusi na uadui wa maadui kwa sababu ya kusimama kwao katika njia ya haki.
Mwakilishi wa Gilan katika Baraza la Wanazuoni aliongeza kuwa: Kauli za amani zinazopamba midomo ya mabeberu ni mbinu za kuufanya Umma kuwa dhaifu, na muqawama wa Iran ni kielelezo kinachotegemea fasihi ya ‘Ashura.
Ziara ya ‘Ashura ni mithili ya kumzuru Mwenyezi Mungu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as), kwa kunukuu riwaya mbalimbali, alisisitiza kuwa: Ziara ya Imam Hussein (as) kwa maarifa ni sawa na kumzuru Mwenyezi Mungu. Imam (as), kwa kujitolea nafsi na wapendwa wake wote, alimfundisha mwanadamu somo la juu kabisa la muqawama.
Alisema kuwa kuhudhuria uwanjani ni sharti la kuelewa kwa kina masaibu ya Karbala na kupata msukumo wa ‘Ashura kwa ajili ya mapambano ya leo.
Alihitimisha kwa kusema kwamba: Mtu wa ‘Ashura sio mtu wa kutishwa, kudhalilishwa au kununuliwa; bali ni lazima asimame dhidi ya wenye jeuri na kupambana nao.
Maoni yako