Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, waandamanaji wa Kiswidi walikusanyika katika mji mkuu wa Sweden na kufanya maandamano kuelekea katika Bunge la Sweden.
Waandamanaji hao walipaza kauli mbiu isemayo: "Israel ni muuaji, ondoka Palestina" na "Sitisha vita, sitisha vita". Waandamanaji hao walikuwa wamebeba bendera za Palestina, na vilevile walitaka kusitishwa kwa mauaji ya kimbari huko Ghaza.
Kwa mujibu wa maafisa wa Wizara ya Afya ya Ghaza, kwa kupuuzia wito wa kimataifa wa kutaka usitishaji mapigano, jeshi la Israel tangia mwezi Oktoba limeendelea kufanya mashambulizi dhidi ya watu wa Ghaza na kuua zaidi ya Wapalestina 56,400 ambapo wengi wao ni wanawake na watoto.
Maoni yako