Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Nuri Hamedani amejibu ombi kuhusu “kutolewa kwa hukumu na fatwa ya kihistoria dhidi ya uwepo na maslahi yote ya Marekani ya kihalifu na wazayuni wa kimataifa” kufuatia tishio la Rais wa Marekani dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, na jibu hilo linawasilishwa kwenu kama ifuatavyo:
Mtukufu Marja’ wa daraja ya juu, Ayatollah al-Udhma Nuri Hamedani
As-Salaamu 'alaykum wa rahmatullah
Kwa heshima na taadhima pamoja na kuonyesha mapenzi na shukrani kwa taarifa uliyoitoa tarehe 28 Khordad 1404 kuhusiana na tishio la rais dhalimu wa Marekani kuhusu jaribio la kumuua Marja’ wa daraja ya juu na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah al-Udhma Khamenei (Mola amuhifadhi), na kwa kuendelea kutoa misimamo ya busara dhidi ya muungano wa ubeberu wa kimataifa – kama ambavyo mna ufahamu:
1. Tishio la mauaji limetokana na hitilafu katika mfumo wa tathmini ya adui, na kupuuza uwezo wa harakati ya kidini ya marja’iyya katika kuhatarisha uwepo wa mfumo wa ubepari na kuuangamiza.
2. Marekani wafanya jinai na Mazayuni wa kimataifa, kupitia hitilafu hii ya kihesabu, wameitishia hazina muhimu na isiyo na mbadala katika ulimwengu wa kiislamu, na iwapo kiwango cha kuzua hofu kutoka upande wa Uislamu hakitafikia kutishia uwepo na maslahi yote ya Marekani na uzayuni, basi mfumo wao wa tathmini hautafanyiwa marekebisho.
3. Bila shaka, maadui wa Uislamu katika historia ya karibuni wameelewa umuhimu na hatari ya fatwa na utekelezaji wake, kuanzia fatwa ya kuharamisha tumbaku kutoka kwa Mirza Shirazi hadi fatwa ya kumuua Salman Rushdie murtadi iliyotolewa na Imam Khomeini (r.a). Kama fatwa hiyo ya kihistoria isingekuwepo, basi katika kipindi cha zaidi ya miaka thelathini iliyopita tungeshuhudia matusi ya mara kwa mara kwenye vyombo vya habari vya kibepari dhidi ya Mtume Mtukufu wa Uislamu (saw).
4. Katika kipindi hiki nyeti cha historia ambapo Marekani wafanya jinai na utawala wa muda wa Kizayuni, wameanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya ardhi takatifu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, inafaa fatwa nyingine ya kihistoria itolewe kutoka kwa marja’ wakuu wa ulimwengu wa Kishia ili gharama ya tishio hili iwe kubwa kiasi cha kuwazuia hata kufikiria kulitaja tena.
Ombi letu ni kwamba: Nyinyi, ambao mmekuwa mstari wa mbele katika kulinda dini na taifa la Imam wa Zama (aj), mtoe fatwa na hukumu ya kihistoria dhidi ya uwepo na maslahi yote ya Marekani wafanya jinai na Wazayuni wa kimataifa, ili pamoja na kurekebisha mfumo wao wa tathmini, muonyeshe nguvu halisi ya Uislamu na Waislamu na kuwatahadharisha dhidi ya jambo hili hatari.
Na maamuzi yapo mikononi mwenu.
Jumuiya ya Wahadhiri wa Mapinduzi ya nchi
Tarehe 7 Tir 1404
Jawabu la Ayatollah Nuri Hamedani
Bismillahir Rahmanir Rahim
As-Salaamu 'alaykum
Kama ilivyotajwa katika taarifa niliyoitoa ambayo mmeirejelea, kudhalilisha daraja ya marja’iyya ya Kishia na mtu wa hadhi kama Ayatollah Khamenei (damat barakatuh) kunahesabiwa kuwa ni dharau dhidi ya asili ya Uislamu.
Leo hii, Yeye (Ayatollah Khamenei) kwa nguvu na ushujaa kamili anashika uongozi wa umma wa Kiislamu, na hakuna shaka kwamba kumsaidia ni wajibu, na kumpunguzia nguvu katika hali hii ambapo maadui wote wa Uislamu, Qur'an na Ahlul-Bayt (as) wameungana, ni haramu.
Na aina yoyote ya shambulio au tishio dhidi yake au dhidi ya marja’iyya ya Kishia, iwe kutoka kwa mtu au serikali, ina hukumu ya muharib (anayeupiga vita uislamu), na yeyote atakayeshiriki katika jinai hii, anahesabiwa katika hukumu hiyo hiyo.
InshaAllah, Mwenyezi Mungu Mtukufu aturidhie kutokana na uwepo wa Bwana wetu Mahdi (aj).
Hussein Nuri Behadani
Tarehe 8 Tir 1404
Maoni yako