Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano hayo makubwa yalifanyika Jumapili katika miji ya Tel Aviv, Yerusalemu na miji mingine, kwa mujibu wa gazeti la "Haaretz". Maandamano haya yalifanyika kufuatia shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran mnamo tarehe 13 Juni na vita vya siku kumi na mbili dhidi ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa kauli ya Israel, mashambulio yao yalilenga vituo vya nyuklia, jeshi pamoja na raia wa kawaida wasiokuwa na silaha. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Kiebrania cha Yerusalemu, operesheni za kijeshi zilizofanywa na Iran kwa ajili ya kujilinda zimesababisha kujeruhiwa takriban Wazayuni 3,400 (idadi kamili ya waliouawa haijatolewa rasmi).
Malalamiko ya wananchi kuhusu kutokuwepo kwa ufanisi katika kuwaokoa mateka yanakuja huku Harakati ya Hamas ikiwa imeshatangaza mara kadhaa utayari wake wa kuwaachia huru mateka wa Kizayuni kwa pamoja kwa masharti ya kusitishwa vita na mauaji ya kimbari ya Israel, kuondolewa kwa jeshi la Israel kutoka Ghaza, na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina.
Kwa mujibu wa wakosoaji wa Israel, Netanyahu anataka kurejea vitani na kuendeleza mauaji ya kimbari huko Ghaza kwa ajili ya kuhifadhi nafasi yake ya uongozi.
Jeshi la Israel, kwa kupuuza miito ya kimataifa ya kutaka sitisho la mapigano, tangu Oktoba 2023 limekuwa likifanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Ghaza na kuwaua zaidi ya Wapalestina 56,400 ambao wengi wao ni wanawake na watoto.
Maoni yako