Jumapili 22 Juni 2025 - 23:58
Sifa za Imam wa zama (aj) Katika Dua

Hawza/ Kwa kuzingatia sifa na tabia za Imam wa zama (a.f) kunaweza kuongeza na kuimarisha zaidi uhusiano wa kiroho na wa ndani kati ya mja na Yeye.

Shirika la Habari la Hawza - katika dua za Mahdawiyyah, Imam wa Zama (aj) ameainishwa kwa sifa ambazo kila moja inafichua sehemu ya utambulisho wake, na husaidia kuimarisha imani juu yake, pamoja na kupandikiza mapenzi na ukaribu zaidi kwa Huyo Bwana Mtukufu.

Miongoni mwa sifa hizo ni:

Alam al-Mansub - عَلَمُ المَنصُوب

Maana yake ni bendera iliyoinuliwa, sifa hii inamaanisha kuwa; uwepo wake mtukufu ni bendera ya uongofu inayowaelekeza wenye kutafuta haki kwenye ukweli. Bila uongozi wake, wanadamu hujikuta wakizama kwenye fitna na upotovu wa kipindi cha ghaiba.

Katika ziyarah ya Aal Yasin tunasoma:

السَّلَامُ عَلَیکَ أَیهَا … العَلَمُ المَنصُوب.

Amani iwe juu yako, ewe bendera iliyoinuliwa.

Safinah al-Najah - سَفینَةُ النَّجاة

Maana yake ni jahazi la wokovu. Kila mtu anayemuamini Imam Mahdi (a.s) na kuifuata amri yake, bila shaka atakuwa miongoni mwa waliookolewa. Hakika, hakuna njia nyingine ya wokovu isipokuwa njia hii.

Katika mojawapo ya ziyara za Imam wa Zama (aj) imekuja hivi:

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی خَلِیفَتِکَ‏ فِی‏ بِلَادِکَ‏ …. سَفِینَةِ النَّجَاةِ.

Ewe Mwenyezimungu! Mteremshie baraka Khalifa wako katika miji yako… ambaye ni jahazi la wokovu.

Warithu Oluminnabiyyin - وَارِثُ عُلُومِ النَّبِیین

Maana yake ni mrithi wa elimu za Manabii. Imam Mahdi (a.s) ni hoja ya mwisho ya Mwenyezi Mungu, na ni kiini cha ujumbe wa Mitume wote. Kulingana na riwaya, elimu zote za kimungu zilizoteremshwa kwa Mitume wa Mwenyezi Mungu zimekusanyika kwa Imam Mahdi (a.s).

Katika ziyarah ya Sardab al-Muqaddas tunamsemesha Imam kwa kusema:

السَّلَامُ عَلَیکَ یا وَارِثَ‏ عُلُومِ‏ النَّبِیین.

Amani iwe juu yako, ewe mrithi wa elimu za Manabii.

Na katika ziyarah ya Aal Yasin, elimu yake imeelezwa kwa maneno haya:

السَّلَامُ عَلَیکَ أَیهَا …. الْعِلْمُ‏ الْمَصْبُوب.

Amani iwe juu yako, ewe chemchemi ya elimu inayomwagika kwa wingi.

Mtakatifu na Aliyeepukana na Kasoro Zote

Uwepo mtukufu wa Imam Mahdi (aj) hauna doa la dhambi wala uchafu wowote wa maasi. Amehifadhiwa na kutakaswa na Allah dhidi ya kila aina ya uovu, kwani yeye ni hoja teule wa Mwenyezi Mungu na muongozi wa wanadamu.

Katika dua ya Imam Ridha (a.s) tunasoma:

عَصَمْتَهُ‏ مِنَ‏ الذُّنُوبِ‏ وَ بَرَّأْتَهُ مِنَ الْعُیوبِ وَ طَهَّرْتَهُ مِنَ الرِّجْسِ وَ سَلَّمْتَهُ مِنَ الدَّنَس.

[Ewe Mungu!] Umemhifadhi dhidi ya dhambi, ukamtakasa dhidi ya kasoro zote, ukamtwahirisha na kila aina ya uchafu, na ukamlinda dhidi ya kila najisi.

Kimbilio na Hifadhi ya Wanadamu

Imam Mahdi (aj) ni hifadhi ya watu wote; ni kimbilio imara kwa walimwengu katika shida, balaa na misiba, ni mlinzi na tegemeo madhubuti.

Katika du'a ya Ahd tunasoma:

واجْعَلْهُ اللَّهُمَ‏ مَفْزَعاً لِمَظْلُومِ عِبَادِکَ وَ نَاصِراً لِمَنْ لَا یجِدُ لَهُ نَاصِراً غَیرَک‏

Ewe Mola! Mja huyu mfanye kuwa ni kimbilio la waja wako wanaodhulumiwa, na msaidizi wa wale wasiokuwa na msaidizi ila Wewe.

Na katika du'a ya Nudba tunasema:

اللَّهُمَّ وَ نَحْنُ عَبِیدُکَ التَّائِقُونَ إِلَی وَلِیکَ المُذَکِّرِ بِکَ و بِنَبیکَ خَلَقْتَهُ‏ لَنَا عِصْمَةً وَ مَلَاذاً، وَ أَقَمْتَهُ لَنَا قِوَاماً وَ مَعَاذا.

Ewe Mola! Sisi ni waja wako wenye shauku kwa mteule wako anayetukumbusha kuhusiana na Wewe na Mtume wako. Ulimuumba kuwa ni kinga yetu, hifadhi yetu, nguzo yetu na kimbilio letu.

Utafiti huu unaendelea…

Imechukuliwa kutoka katika kitabu “Nageen-e-Afarinesh” humu ikifanyiwa mabadiliko kiasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha