Jumapili 22 Juni 2025 - 23:45
Wananchi wa India wapinga vikali kauli za uchochezi zilizo tolewana Trump

Hawza/ Wakati wa maandamano ya kupinga uonevu huko Lucknow, waandamanaji walichoma moto picha za Benjamin Netanyahu na Donald Trump pamoja na bendera ya utawala wa Kizayuni, wakionesha ghadhabu yao dhidi ya uhalifu unaofanywa na Israel na vitisho vya Marekani dhidi ya Ayatollah Khamenei.

Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, maandamano makubwa ya kupinga shambulio la kigaidi lililofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, pamoja na vitisho vya Rais wa Marekani vya kutaka kumuua Kiongozi Mkuu wa Waislamu wa Kishia, Hadhrat Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (hifadhi ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake), yamefanyika katika msikiti wa Asifi mjini Lucknow, India.

Katika maandamano hayo, waandamanaji walitoa kauli kali dhidi ya ugaidi wa Israel unaoungwa mkono na Marekani, huku wakizichoma moto picha za Rais wa Marekani pamoja na ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni na pia bendera ya Israel. Waliimba pia kaulimbiu ya kuiunga mkono Iran na uongozi wa kidini (marjaa).

Aidha, waandamanaji walilalamikia vyombo vya habari vya mitazamo ya upande mmoja nchini India, ambavyo vinaendelea kumvunjia heshima Ayatollah Khamenei, na wakavitaka kusitisha mwelekeo huo wa chuki na uchochezi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha