Jumatano 12 Agosti 2026 - 01:15
Muqawama utaendelea kuwa kisu katika kifua cha kila dhalimu na mvamizi

Hawzah/ Hujjatul-Islam Sayyid Shukr amesisitiza kwamba; Muqawama utaendelea kuwa kisu katika kifua cha kila dhalimu na mvamizi; wale walioikomboa Kusini wanaweza kuikomboa tena.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya 40 tangia kupaa kwa Shahidi Mujahid Hassan Mustafa Lazqani, anayejulikana kwa jina la “Adam”, Hizbullah pamoja na familia ya shahidi huyo waliandaa hafla kubwa katika Husainia ya Imam Sadiq (as) mjini Hermel.

Katika hafla hiyo walihudhuria Hujjatul-Islam Sayyid Faisal Shukr, Naibu Msimamizi wa Mkoa wa Biqa‘ wa Hizbullah, wanazuoni wa dini, familia za mashahidi, viongozi na watu mashuhuri, pamoja na umati mkubwa wa wakazi wa Biqa‘.

Hujjatul-Islam Sayyid Shukr alisema: Muqawama utaendelea kuwa kisu katika kifua cha kila dhalimu na mvamizi; wale walioikomboa Kusini wanaweza kuikomboa tena, na wale waliutetea heshima na utu wa Lebanon wanaweza kulifanya hilo tena.

Aliendelea kusema: Mashahidi wetu ni wateule ambao Mwenyezi Mungu amewachagua kwa ajili ya cheo hiki, nao ni akiba na mtaji wa njia hii. Ahadi yetu kwao ni kwamba kamwe, hata kwa muda wa kupepesa kwa jicho, hatutakuwa kama wale walioacha dini yao, Muqawama wao, utukufu wao na heshima yao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha