Shirika la Habari la Hawza - Jumuiya na taasisi za kisayansi pamoja na Tume ya Haki za Binadamu za Hawza wametoa tamko kali la kulaani matamshi yasiyo na uwajibikaji, batili, na kinyume na misingi yote ya kimataifa na kibinadamu yaliyotolewa na Rais wa Marekani.
Tamko hilo, ambalo ni kwa niaba ya wanazuoni, wanasheria, watafiti na wanazuoni wa dini katika taasisi hizo, linaeleza yafuatayo:
بسم الله الرحمن الرحیم
«وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّهِ النَّاسَ بَعْضَهُمْ بِبَعْضٍ لَهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَ بِیَعٌ وَ صَلَوَاتٌ وَ مَسَاجِدُ یُذْکَرُ فِیهَا اسْمُ اللَّهِ کَثِیرًا وَلَیَنْصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ یَنْصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِیٌّ عَزِیز.»
"Na lau si kwamba Mwenyezi Mungu anawakinga baadhi ya watu kwa baadhi yao, basi hakika zingeharibiwa sinagogi, makanisa, masinagogi na misikiti ambayo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa sana na bila shaka Mwenyezimungu humsaidi yule anae msaidia yeye, hakika ya mwenyezimungu ni mwenye nguvu mtukufu." (Surat Al-Hajj: 40)
Viongozi wa kidini na wanazuoni ni kioo cha utambulisho wa mataifa ya Kiislamu na jamii za kibinadamu. Kuwadhuru wao ni sawa na kushambulia imani na hisia za mamilioni ya watu, na ni tishio kwa uwepo wa kiroho na kistaarabu wa jamii.
Kwa msingi huu, Jumuiya za Hawza kwa niaba ya wanazuoni na wataalamu wa sheria, zinasisitiza mambo yafuatayo:
1. Uvunjaji wa Misingi ya Sheria za Kimataifa na Katiba ya Umoja wa Mataifa
Vitisho vya kuwaua viongozi wa kisiasa na kidini – hususan maafisa wa juu wa nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa – ni ukiukaji wa wazi wa kanuni kuu za sheria za kimataifa. Hii ni kinyume na Kifungu cha 4 cha Ibara ya 2 ya Katiba ya Umoja wa Mataifa, na pia ni kinyume na misingi ya haki za kibinadamu na ulinzi wa viongozi wa kiraia katika nyakati za amani au vita.
2. Kuchochea Chuki na Kuchafua Hisia za Umma
Vitisho kama hivi ni mfano wa wazi wa uchochezi wa chuki, vinavyoudhi hisia za kidini za Waislamu na hata mataifa mengine ya huru na ya heshima. Kifungu cha 2 cha Ibara ya 20 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa unakataza wazi aina yoyote ya uchochezi wa chuki ya kitaifa, kidini au kikabila. Vitendo hivi vina uwezo wa kusababisha machafuko makubwa ya kimataifa.
3. Wajibu wa Kisheria kwa Wale Wanaotoa Vitisho vya Mauaji
Sheria za kimataifa – ikiwemo Mkataba wa Roma wa 1998 – zinahesabu kuchochea mauaji au ugaidi dhidi ya viongozi wa dini au wa kisiasa kama kosa la jinai linalowajibisha adhabu ya kisheria. Vitendo hivi vinafuta kinga yoyote ya kidiplomasia kwa wahusika.
4. Hitaji la Majibu ya Haraka kutoka katika Taasisi za Kimataifa na Kikanda
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN na taasisi nyingine za haki za binadamu wanapaswa kuchukua msimamo mkali na wa wazi dhidi ya vitisho hivi, kabla havijawa mtindo wa kawaida wa viongozi wa kibeberu.
5. Haki ya Iran ya Kujilinda Kwa Mujibu wa Kifungu cha 51 cha Katiba ya Umoja wa Mataifa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina haki ya asili ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya aina yoyote, kwa kutumia rasilimali zake zote – iwe ni kijeshi au zisizo za kijeshi – kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Hitimisho:
Jumuiya na taasisi za kisayansi na Tume ya Haki za Binadamu na Hawza zinalaani vikali matamshi na vitisho visivyo na uhalali vya Rais wa Marekani, na zinazitaka taasisi za kidiplomasia za Iran, taasisi za kimataifa na watu huru duniani kote kusimama kidete dhidi ya dhulma hizi za wazi na za kinyama.
Maoni yako