Jumamosi 28 Juni 2025 - 13:42
Maombolezo ya Muharram ya mwaka huu yafanyike kwa namna ya adhama zaidi kuliko miaka iliyopita / Hawza na maulamaa daima wamesimama imara juu ya ahadi yao kwa raia

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza amesisitiza kuwa: Maombolezo ya mwezi wa Muharram mwaka huu yanapaswa kufanyika kwa namna ya adhama zaidi kuliko zamani kwa lengo la kuimarisha hamasa ya Ashura na kubainisha ujumbe wa heshima na unaopinga dhulma wa Imam Husain, na vielelezo vya kishujaa vya Ashura katika mapambano dhidi ya dhulma na unyonyaji, pamoja na kusimama imara juu ya maadili ya dini viwekwe wazi zaidi mbele ya macho ya walimwengu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah A‘raafi, Mkurugenzi wa Hawza, katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa mwezi wa Muharram alisisitiza kuwa: Maombolezo ya mwezi wa Muharram ya mwaka huu yanapaswa kufanyika kwa namna ya adhama zaidi kuliko miaka iliyopita kwa lengo la kuimarisha hamasa ya Ashura na kubainisha ujumbe wa heshima na unaopinga dhulma wa Imam Husain, na vielelezo vya kishujaa vya Ashura katika mapambano dhidi ya dhulma na uonevu pamoja na kusimama imara juu ya maadili ya kidini viwekwe wazi zaidi mbele ya macho ya walimwengu.

Matini ya ujumbe ni kama ifuatavyo:

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمٰنِ الرحيم
الحمدلله قاصم الجبارين ومدرك الهاربين، والصلاة والسلام على المصطفى واله الاطهار

As-salaamu ‘alayka ya Aba ‘Abdillah (as)

Mara nyingine tena, Ashura yenye damu na uhai imewadia, na bendera za maombolezo ya Bwana wa Mashahidi zimepeperushwa, ndani ya Iran na ulimwenguni kote, matukio ya maombolezo ya Abā ‘Abdillah al-Hussein (as) yameandaliwa, na taa ya hamasa na shauku ya Ashura imewashwa. Masomo ya madhehebu ya Ashura yanahuishwa, na vikao vya Karbala vinapata uhai kwa ushiriki mkubwa wa umma, uwepo wa vijana wa Hussein, vikundi vya maombolezo, pamoja na mchango mkubwa wa wanazuoni, wahubiri wa dini, na wenye mimbar ya Hussein (as) katika kuleta hamasa na kuongeza maarifa.

Hata hivyo, Ashura na Arubaini ya mwaka huu vina sura na mandhari tofauti. Hii ni kwa sababu tumeshuhudia baada ya karibu miaka miwili ya ukatili wa kipumbavu wa Wazayuni wamwagaji wa damu, Marekani na madhalimu wa kimataifa, mkono wa Mungu umetokea kupitia taifa jasiri la Iran. Mapinduzi tukufu ya Kiislamu baada ya kung'ara kwa harakati mwezi Khordad 1342 (1963) na ushindi tarehe 22 Bahman 1357 (1979) na ushindi katika vita vya kujihami mwaka 1367 (1988), sasa yameingia katika awamu mpya.

Kwa uongozi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (Mola amuhifadhi), na kwa mshikamano wa Marjaa wakubwa (d'ama dhilluhum), wanazuoni mashuhuri, wanavyuoni wa Hawza na vyuo vikuu, pamoja na mshikamano wa tabaka na makundi yote ya taifa la Iran na muhimili wa muqawama, na kwa kujitolea kwa vikosi vya kijeshi vya nguvu na jasiri pamoja na mshikamano wa kitaifa na ushiriki wa watu wote, tishio kubwa na hatari limegeuzwa kuwa ushindi wa Mwenyezi Mungu uliojaa fahari.

Njama za kishetani za maadui za kuivunja ngome ya muqawama, kushinda mfumo wa Kiislamu, kuvunja uwezo wa kiroho na wa kijamii wa taifa, pamoja na kuharibu nguvu ya ulinzi ya Iran, zimefutwa kabisa. Nafasi ya kihistoria imeibuka, nguvu mpya katika eneo na duniani imejidhihirisha na kuimarika. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, mawimbi ya dhoruba hii yataendelea katika historia ya Iran, Asia ya Magharibi na dunia.

Kwa kweli, roho mpya ya matumaini imevuma katika ulimwengu wa Kiislamu na kwa wanyonge, na uadui wa madhalimu amedhihirika zaidi, na nguvu laini na ngumu ya Iran na Mapinduzi ya Kiislamu imejitokeza kwa uwazi zaidi.

Mimi, kwa niaba ya Hawza, ninatoa shukrani za dhati kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Marjaa wakubwa wa Taqleed, na taifa la Iran ambalo daima liko mstari wa mbele, hasa vikosi vya kijeshi vya jihadi, na ninatoa pongezi kwa ushindi huu wa kuongozwa na uongozi wa kiongozi mkuu na ushirikiano wa watu.

Nikiwa katika fursa ya kuadhimisha Ashura na Arubaini ya Imam Hussein (as), nitaelezea nukta kadhaa:

Maombolezo ya Muharram ya mwaka huu yanapaswa kufanyika kwa namna ya adhama zaidi kuliko miaka iliyopita kwa lengo la kuimarisha hamasa ya Ashura na kubainisha ujumbe wa heshima na unaopinga dhulma wa Imam Hussein, na vielelezo vya kishujaa vya Ashura katika mapambano dhidi ya dhulma na uonevu pamoja na kusimama imara juu ya maadili ya kidini viwekwe wazi zaidi mbele ya macho ya walimwengu.

Ashura ni madhehebu ya kina, chanzo cha mwangaza, na chenye vipengele na masomo mengi katika njia ya kumtakasa mwanadamu na jamii. Daima imekuwa ni dhamana ya uendelevu wa ujumbe wa Uislamu na maadili ya juu, na imekuwa ni uti wa mgongo wa heshima na uhuru wa Iran. Mwenge huu lazima uendelee kuwaka kwa nguvu zaidi. Ni jukumu la wahubiri wa dini, haia za maombolezo, na taasisi za kiutamaduni kufafanua mafundisho ya kimungu, kulea vijana, kuimarisha itikadi za kidini, tabia njema, na utambulisho wa Kiislamu na wa kitaifa kwa mujibu wa kielelezo hiki chenye mwangaza.

Mapinduzi ya Kiislamu yana hazina ya thamani ya maarifa na mtazamo mpana wa ustaarabu. Taifa la Iran likiwa na historia ndefu na ya fahari, kwa kufuata uongozi wa Imam Khomeinī (quddisa sirruh), liliyaasisi mapinduzi haya, na kwa juhudi kubwa ya taifa hili adhimu, vijana wake mashujaa, muhimili wa muqawama, na wapigania uhuru wa dunia, limeiweka katika njia ya maendeleo. Mtazamo huu wa juu lazima uendelee kufahamika, kufasiriwa, na kulindwa. Ni jukumu la maulamaa na watu wote wa kazi za kiutamaduni na kielimu ndani na nje ya Iran kutoa mwanga katika uwanja huu.

Kutokana na kusimama imara na mapambano haya, mafanikio mengi ya kimwili na ya kiroho yamepatikana kwa nchi yetu katika ngazi ya kikanda na kimataifa. Mipango yote tata na pana dhidi ya uhuru na heshima ya Kiislamu na kitaifa ya Iran na Mapinduzi yamefutwa. Sote tunapaswa kufafanua haya kwa uelewa wa kina, lugha ya kuvutia, na ufafanuzi wa kisanaa kwa tabaka mbalimbali za watu. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, katika vita hivi vya siku kumi na mbili, Umma wa Kiislamu na muhimili wa mapambano kupitia msimamo na mapambano ya kishujaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, umepata uhai mpya. In shaa Allah kwa kuhifadhi na kuimarisha utayarifu huu katika uwanja wa mapambano, kufikia kilele cha ushindi dhidi ya muungano wa ukafiri na ubeberu kutakuwa karibu zaidi.

Taifa adhimu la Iran na vikosi vyake vya kijeshi vya nguvu walikuwa tayari kwa vita vya muda mrefu, na hivi sasa wamesimama imara zaidi kuliko wakati wowote katika njia ya kulinda heshima ya Kiislamu na ya kitaifa.

Ukurasa huu wa kipekee wa historia ya Iran na Uislamu lazima uzingatiwe katika programu za Ashura, na pia katika mfumo wa kiutamaduni, kielimu na kijamii, lazima usimuliwe kwa njia sahihi.

Hivi sasa ni muhimu kwa vyombo vitatu vya dola, vikosi vya kijeshi, vyombo vya kijasusi na vya kiusalama, pamoja na taasisi za kiutamaduni na kielimu, na viongozi wote wa sekta mbalimbali, kuchukua hatua kwa kasi na kwa umakini katika kutathmini maeneo yenye nguvu na udhaifu, kupanga mikakati ya kurekebisha mapungufu, na kuimarisha zaidi miundombinu ya kiulinzi, kiusalama, kiroho na ya kimaadili ya jamii. Pia wazingatie haki ya kujihami kwa halali na kudai haki za taifa.

Tunatarajia kutoka katika serikali za ukanda huu, kuiga na kujifunza kutokana na mapambano haya yenye taathira ya kina na ya kujivunia ya taifa la Iran, ziachane na woga na hofu dhidi ya Marekani na vibaraka wake wa wabeberu, na kwa mshikamano na umoja zisimame kwa pamoja mbele ya ngome dhaifu ya mfumo wa kimabavu hadi ushindi kamili. Ziwatetee wanyonge wa Palestina. Maadui madhalimu wajue kuwa zama za kupayuka kwa ujeuri zimekwisha, dunia mpya iko katika hatua ya kuchomoza, na kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, orodha ya dhulma zao itaangamizwa, na Iran na Mapinduzi ya Kiislamu yataendelea kwenye njia ya maendeleo na ukamilifu.

Mwisho, ninasisitiza kuwa Hawza na taasisi zake pamoja na maulamaa walioko mstari wa mbele daima wamesimama imara juu ya ahadi yao kwa watu, na kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu neema hii kubwa itahifadhiwa. Katika matukio ya hivi karibuni kama ilivyokuwa katika misukosuko mingine, kwa kupanga mikakati na kuunda vituo vya operesheni, wamekuwa bega kwa bega na wananchi wapendwa, na wametumia juhudi zao zote katika kutekeleza malengo ya mfumo mtukufu wa Kiislamu na kulinda taifa la Iran kama ilivyokuwa daima, na wataendelea na njia hii.

وآخر دعوانا أن الحمد لله رب العالمين

Alireza A‘raafi
Mkurugenzi wa Hawza Iran
28 Dhul-Hijja 1446 Hijria Qamariyya

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha