Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mheshimiwa Saira Ibrahim, mwanachama mwandamizi wa kitengo cha wanawake cha Baraza la Umoja wa Waislamu wa Gilgit-Baltistan, katika hotuba yake alisisitiza kuwa ushindi wa hivi karibuni wa mfumo wa Wilayat Faqih na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kama kofi kali lililopigwa usoni mwa wanafiki, na wale ambao kwa nje ni simba lakini kwa ndani ni panya.
Aliongeza kwa kusema: Ushindi huu si tu mafanikio ya kijeshi, bali ni ushindi wa imani, hamasa ya kishujaa, na fikra ambayo imeleta changamoto dhidi ya ubeberu.
Mheshimiwa Saira Ibrahim alisema pia: Hili ni tukio la kihistoria ambapo dunia imeona kwamba taifa ambalo kiongozi wake ni Waliyyu al-Faqih na damu ya Karbala inapita katika mishipa yake, haliwezi kushindwa kamwe, bali huwa muundaji wa historia.
Akiashiria mafunzo ya Karbala, alisema kwamba: Taifa la Iran kwa kufuata mafundisho ya Karbala limefanya jambo ambalo kwa miongo kadhaa hakuna taifa lililoweza kulifanya na wala halitaweza kufanya.
Maoni yako