Jumanne 24 Juni 2025 - 22:46
Hadhi na Vyeo vya Imamu Mahdi (aj) katika Dua

Hawzah/ Kuzingatia vyeo na nafasi za Imamu wa zama (aj) katika ulimwengu kunaweza kuwa sababu ya kumkaribisha zaidi mja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, kupitia kusoma na kutafakari dua za Mahdawiyya, sura ya wazi ya hadhi na vyeo vya Imam huwekwa bayana, na mlango wa maarifa hufunguliwa kwa wale wanaomwamini, hapa tunanukuu baadhi ya vyeo hivyo:

خليفة الله، حجة الله
Khalifa wa Mwenyezi Mungu, Hoja wa Mwenyezi Mungu

Katika Ziyārah ya Al Yāsīn imekuja:

السَّلَامُ عَلَیکَ یا خَلِیفَةَ اللَّهِ وَ نَاصِرَ حَقِّهِ‏، السَّلَامُ عَلَیکَ یا حُجَّةَ اللَّهِ وَ دَلِیلَ إِرَادَ.

Amani iwe juu yako, ewe Khalifa wa Mwenyezi Mungu na msaidizi wa haki Yake. Amani iwe juu yako, ee Hujja wa Mwenyezi Mungu na mwongozo wa irada Yake.

Ni dhahiri kuwa nafasi ya kuwa Khalīfatullāh na Hujjatullāh ni miongoni mwa hadhi tukufu mno ambazo Mwenyezi Mungu amempa Imamu Mahdi as. Katika cheo hiki, yeye ni wa kipekee na hana mfano katika zama zake.

باب الله، سبيل الله
Mlangonwa Mwenyezi Mungu, Njia ya Mwenyezi Mungu

Katika Ziyārah ya Āl Yāsīn tunasoma:

السَّلَامُ عَلَیکَ یا باب الله.

Amani iwe juu yako, ewe mlango wa Mwenyezi Mungu.

Na katika Ziyārah ya Sāhib al-Amr (as) tunasoma:

السَّلَامُ عَلَیکَ یا سَبِیلَ اللَّهِ الَّذِی مَنْ سَلَکَ غَیرَهُ‏ هَلَک.

Amani iwe juu yako, ewe njia ya Mwenyezi Mungu ambayo yeyote anayefuata isiyo hiyo huangamia.

Kauli ya “mlango wa Mungu” inaonyesha ukweli huu kuwa yeyote anayetaka kumfikia Mwenyezi Mungu, kumtii na kupata radhi Zake, ni lazima apitie njia ya kuamini na kuifuata imani ya Imamu Mahdi (as) pamoja na utiifu kamili kwake. Na kauli ya “njia ya Mungu” nayo inaeleza jambo hilo hilo kwamba njia pekee ya kumfikia Mungu na kupata ukaribu Wake ni imani, yakini na utiifu kwa walii wa Mungu, yaani Imamu wa Zama (as).

ميثاق الله، وعد الله
Kiaga cha Mwenyezi Mungu

Katika Ziyārah ya Āl Yāsīn imeandikwa:

السَّلَامُ عَلَیکَ یا مِیثَاقَ‏ اللَّهِ‏ الَّذِی‏ أَخَذَهُ وَ وَکَّدَهُ، السَّلَامُ عَلَیکَ یا وَعْدَ اللَّهِ الَّذِی ضَمِنَه.

Amani iwe juu yako, ewe ahadi ya Mwenyezi Mungu ambayo Yeye aliichukua kutoka kwa viumbe na akaithibitisha. Amani iwe juu yako, ewe ahadi ya Mungu ambayo Yeye mwenyewe ameihakikisha.

Kauli ya “ميثاق الله” ina maana kwamba Imamu Mahdi (as) ni mfano kamili wa ahadi na kiaga ambacho Mwenyezi Mungu alikichukua kwa waja Wake. Ahadi ya watu kwa Imamu Mahdi (as) ni mithili ya kushikamana kwao na dini nzima ya Mwenyezi Mungu, kumwacha au kujiweka mbali naye ni sawa na kuvunja ahadi zote za Mwenyezi Mungu.

Kauli ya “وعدالله” nayo ina maana kwamba Imamu Mahdi (as) ndiye mfano wa wazi wa ahadi ya Mungu iliyotajwa katika Qur’an kuhusu utawala wa watu wema na kusambaa kwa maadili na mema duniani. Yeye ndiye mteule mkubwa wa Mwenyezi Mungu ambaye kudhihiri kwake kutatekeleza malengo ya manabii wote na wateule, na kufufua sheria na kitabu cha mbinguni. Naam, yeye ni ahadi iliyohakikishwa na Mwenyezi Mungu na mteule wa kweli wa vitabu vyote vya mbinguni ambaye hakuna kitu kitakachozuia kudhihiri kwake.

عين الله الناظرة
Jicho la Mwenyezi Mungu lenye kutazama

Katika dua iliyopokelewa kutoka kwa Imamu Ridha (as) imekuja:

وَعَینِکَ‏ النَّاظِرَةِ عَلَی بَرِیتِکَ وَ شَاهِدِکَ عَلَی عِبَادِک.

Na macho Yako yanayoyaangalia viumbe Wako, na shahidi Wako juu ya waja Wako.

Maneno haya yanaonyesha kuwa Imamu Mahdi (as), kama hujjah na mwakilishi wa Mwenyezi Mungu, pia ni mlinzi wa Mwenyezi Mungu. Matendo ya watu, ya dhahiri na ya siri, hayafichiki kwake; bali yeye ni shahidi na mlinzi juu ya kila tendo. Imani katika ukweli huu husaidia sana katika kulea nafsi, kujisafisha na kuwa watu wa uchamungu.

Katika kauli kutoka kwa Imamu Mahdi as imekuja kuwa amesema:

فَإِنَّا نُحِیطُ عِلْماً بِأَنْبَائِکُمْ وَ لَا یعْزُبُ عَنَّا شَی‏ءٌ مِنْ أَخْبَارِکُم‏.

“Hakika elimu yetu imezunguka habari zenu, na hakuna chochote katika habari zenu kilichofichika kwetu.” (al-Iḥtijāj, j. 2, uk. 495)

Utafiti huu unaendelea...

Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho "Negin-e Āfarinish" huku ikifanyiwa mabadiliko kiasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha