Alhamisi 19 Juni 2025 - 00:23
Radi amali ya Ayatollah al-‘Udhma Nouri Hamedani kutokana na Shambulizi lililofanywa na Utawala wa Kizayuni dhidi ya Shirika la Habari na Matangazo la Iran Seda wa Sima (media)

Hawza/ Hadhrat Ayatollah al-‘Udhma Nouri Hamedani ameeleza kuwa: Katika vita yeyote ile shirika la habari halivamiwi, lakini utawala haramu wa Kizayuni leo hii wamewauwa kishahidi mamia ya waandishi wa habari, na jana pia walivamia bila ya huruma katika kituo cha kutolea habari Irani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya  Ayatollah al-‘Udhma Nouri Hamedani akielezea jinai zilizo fanywa na utawala haramu wa Israeli ni kama ifuatavyo.

Katika jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

Siku hizi tunashuhudia uvamizi wa kinyama unaofanywa utawala dhalimu wa Kizayuni dhidi ya nchi yetu pendwa ya Kiislamu, Iran.

Utawala huu uliundwa kwa msingi wa uzushi na udanganyifu, na kwa hivyo hudhani kuwa uwepo wake unategemea kushambulia mataifa mengine. Leo anashambulia watu wasio na hatia na wasio na silaha wa Ghaza, kesho Lebanon ya kusini na Syria, na sasa Iran, na baada ya hapo nchi nyingine tena. Uvamizi wake hauna mipaka, na kinyume na kanuni za kimataifa, unashambulia maeneo ya makazi ya raia na hospitali, ukionesha wazi hulka yake ya kinyama na ya kiistikbari.

Katika vita yoyote, waandishi wa habari hawashambuliwi kwa kuwa wao ni wakusanya habari na waripoti wa matukio. Hata hivyo, utawala huu hadi leo ameshawaua mashahidi mamia miongoni mwa waandishi wa habari, na jana pia, kwa kitendo kisicho na uungwana, ulishambulia rasmi Kituo cha Taarifa cha Iran, na kwa wazi ukaonesha uso wake wa kinyama. Hata hivyo, wafanyakazi waaminifu wa Shirika la Utangazaji la Taifa Seda wa Sima waliendelea kwa nguvu kubwa na kazi yao.

Katika siku hizi, maneno ya Imam Khomein (ra) yanazidi kudhihirika:
"Watu wetu ni bora kuliko watu wa mwanzo wa Uislamu." Dunia imeona jinsi ambavyo watu hawa, licha ya changamoto walizonazo, walivyodhihirisha umoja na mshikamano wao. Na hata baadhi ya makundi ya kisiasa ambayo yalikuwa na malalamiko, katika uso wa adui wameungana kwa mshikamano.

Umoja huu na hali hii ya kuwa wamoja lazima iendelee, na ni lazima watu waendelee kumuunga mkono Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ambaye kwa hekima na busara anaongoza njia hii. Vilevile msaada na uungaji mkono kwa vikosi vya kijeshi pamoja na mashirika ya ujasusi na usalama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni jambo la lazima na muhimu sana, ili – in shaa Allah – waweze kwa uthabiti zaidi kuujibu uvamizi huu wa madhalimu, na kulipiza kisasi kwa ajili ya damu ya watu wasio na hatia, pamoja na mashujaa wetu na wanasayansi wetu waliouawa.

(یَا أَیُّهَا الَّذِینَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ یَنصُرْکُمْ وَیُثَبِّتْ أَقْدَامَکُمْ)

"Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu." (Qur’an 47:7)

Hussein Nouri Hamedani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha