Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei katika kikao na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Kongamano la Kitaifa la Mashahidi waokoaji, aliwatambua waokoaji kama ni mfano wa sifa za kibinadamu na upendo kwa wanadamu, na huku akisisitiza juu ya umuhimu wa kuendelezwa kwa roho ya kujitolea na huruma ndani ya taifa la Iran, kuhusiana na kutengeneza utamaduni alisema: Kinyume cha utu huu, ni jinai na unyama unaofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza pamoja na uungaji mkono wa Magharibi kwa jinai hizo; na kusimama dhidi ya umwagaji damu huu na upande wa batili ni wajibu wa wote.
Ayatollah Khamenei alisema: Waokoaji walikuwa katikati ya mvua ya risasi, lakini wao walikuwa wakifikiria tu kuwaokoa wengine na si kujilinda wao wenyewe, na roho ya ajabu ya kujitolea ndani yao ilikuwa kubwa kiasi kwamba mara nyingine walikuwa wakisaidia hata majeruhi waliokuwa mateka wa maadui, tabia hii ni kinyume kabisa na dunia isiyo na ubinadamu.
Kiongozi wa Mapinduzi alitaja kwamba kinyume cha roho ya kujitolea na kutoa misaada ni hulka na mienendo ya kinyama inayofanywa na wahalifu Kizayuni katika kushambulia magari ya wagonjwa, kubomoa hospitali, na kuua wagonjwa pamoja na watoto wasio na ulinzi, na akasema: Leo dunia inatawaliwa na wanyama wenye sura ya binadamu, na Jamhuri ya Kiislamu inajiona kuwa na wajibu wa kusimama imara mbele ya unyama huu na umwagaji damu wa kipumbavu unaofanywa na madhalimu hao.
Ayatollah Khamenei huku akisisitiza kuwa kulaani jinai dhidi ya raia wasio na hatia ni wajibu wa wote, aliongeza: Hisia hizi za uwajibikaji ndizo zinazochochea harakati na kuendeleza mwangaza wa matumaini ndani ya nyoyo, na hakika zimewafanya maadui kama Wamagharibi kusimama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Kwani lau sisi tungeacha kulalamikia unyama wao, wao wasingekuwa na uadui na sisi.
Yeye alieleza kuwa tatizo kuu la mabeberu wa Magharibi ni kukataliwa kwa utamaduni wao batili na Jamhuri ya Kiislamu, na akasema: Batili ni yenye kuhukumiwa kuangamia na kutoweka. Bila shaka, ili jambo hili litimie, lazima kuwe na hatua na kusimama kidete, na kuepukwe hali ya kukaa kimya, kukimbia, kutabasamu au kusifu batili, vitendo ambavyo husababisha batili izidi kusonga mbele.
Maoni yako