Shirika la Habari la Hawza - Mojawapo ya maswali ambayo daima huwavutia na kuwashughulisha watu wengi ni hili: Je, Imam wa Zama "‘alayhis-salaam" atadhihiri lini? Na je, kuna wakati ulioainishwa rasmi kwa ajili ya kudhihiri kwake?
Jibu ni kuwa, kwa mujibu wa kauli za viongozi wa dini, wakati wa kudhihiri ni jambo lililofichika kwa watu.
Imam Swadiq "alayhis-salaam" kuhusiana na hili amesema:
«کَذَبَ اَلْمُوَقِّتُونَ، مَا وَقَّتْنَا فِیمَا مَضَی، وَ لاَ نُوَقِّتُ فِیمَا یَسْتَقْبِلُ.»
Wenye kuweka wakati wamesema uongo, Sisi hatukuwahi kuainisha wakati [wa kudhihiri] zama zilizopita, na wala hatuta ainisha wakati zama zijazo. (Al-Ghaybah, Shaykh Tusi, Juzuu ya 1, uk. 426)
Hivyo basi, wale wanao bainisha wakati maalumu kwa ajili ya kudhihiri ni wadanganyifu na waongo. Hili limeelezwa kwa kusisitizwa katika riwaya mbalimbali.
Imam Baaqir – ‘alayhis-salaam– pia alimwambia mmoja wa maswahaba wake aliyemuuliza kuhusu wakati wa kudhihiri:
«کَذَبَ الوَقّاتونَ، کَذَبَ الوَقّاتونَ، کَذَبَ الوَقّاتونَ.»
Wenye kuainisha wakati wanasema uongo! Wenye kuainisha wakati wanasema uongo! Wenye kuainisha wakati wanasema uongo! (Al-Ghaybah, Shaykh Tusi, Juzuu ya 1, uk. 425)
Kutokana na riwaya kama hizi, inafahamika wazi kwamba daima wamekuwepo watu walio bainisha wakati wa kudhihiri kwa kutumia nia za kishetani, na watu wa aina hiyo wataendelea kuwepo hata baadaye. Hivyo basi, viongozi maasumu – ‘alayhimus-salaam – wamewataka Mashia wao wasiwapuuzie wenye kuainisha wakati, bali wawakanushe na wawakanushe wazi.
Imam Swadiq – ‘alayhis-salaam – kuhusiana na hili alimwambia mmoja wa maswahaba wake:
«مَنْ وَقَّتَ لَکَ مِنَ اَلنَّاسِ شَیْئاً فَلاَ تَهَابَنَّ أَنْ تُکَذِّبَهُ، فَلَسْنَا نُوَقِّتُ لِأَحَدٍ وَقْتاً.»
Mtu yeyote atakayekuambia jambo lolote kuhusiana na kuainisha wakati, usihofu kumkanusha, kwani sisi hatuja bainisha wakati kwa yeyote. (Al-Ghaybah, Shaykh Tusi, Juzuu ya 1, uk. 426)
Utafiti huu unaendelea...
Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiiywacho “Negin-e Āfarinesh”, huku ikifanyiwa marekebisho kiasi
Maoni yako