Kulingana na kundi la Tarjama la Shirika la Habari la Hawza, wasomi hao watatu wa Pakistan walikuwa wakielekea nchini mwao kuhubiri (kufanya Tabligh) wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan walipotoweka. Kufikia sasa, hakuna taarifa yoyote iliyochapishwa kuhusu hali zao na mahali walipo.
Kutekwa nyara kwa Wanazuoni hao kumeamsha hasira za wasomi wa Pakistani na watu mashuhuri wa kisiasa. Sheikh Nisar Mehdi, Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Shagar, alisema katika kujibu hatua hii: Hatua hii haramu ni ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi.
Ikiwa wasomi (wanazuoni) hawa watakuwa na mashtaka, basi wahukumiwe katika Mahakama ya Sheria, vinginevyo waachiliwe mara moja. Vinginevyo, maandamano makubwa yatafanyika kote Pakistan na Serikali itawajibika kwa matokeo yake.
Maoni yako