Jumapili 23 Februari 2025 - 15:55
Ujumbe wa Hafla ya Mazishi ya Mujahid mkubwa, Shahidi Syed Hasan Nasrullah na Shahidi Syed Hashem Safiyyuddin

Ayatollah Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake kwa mnasaba wa mazishi na maziko ya Shahidi Mkubwa wa Mujahidina Syed Hassan Nasrullah na pia Syed Hashem Safiyyu al-Din amesisitiza akiwatukuza Mashahidi hawa wawili na wakubwa wa Upinzani (Muqawamah), ambapo amesema: Adui anapaswa kujua kwamba Upinzani (Muqawamah) dhidi ya unyang'anyi , dhulma, ukandamizaji na kiburi (uistikbari) -yote hayo- hayajaisha (na hayaishi) na yataendelea hadi kufikia mahala panapokusudiwa (hadi kufikia hatima). Nakala (andiko) ya ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ni kama ifuatavyo.

Shirika la habari la Hawza - Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

﴿وَلِلّٰهِ العِزَّةُ وَ لِرَسولِهِ وَ لِلمُؤمِنينَ وَلٰکِنَّ المُنافِقينَ لا يَعلَمون.﴾

"Lakini (uwezo, utukufu na) nguvu ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini, lakini wanafiki hawajui". (Surah al-Munafiqun, Aya ya 8)

Mujahid Mkubwa na Kiongozi wa Upinzani (Muqawamah) katika eneo la kikanda, Hazrat Syed Hassan Nasrullah (Mwenyezi Mungu amnyanyue juu kwa daraja yake), sasa yuko kwenye kilele cha Utukufu wake. Mwili wake safi utazikwa katika ardhi ya Jihad kwa jina la Mwenyezi Mungu, lakini roho yake na njia yake itakuwa tukufu zaidi kuliko hapo awali, Insha Allah (Mwenyezi Mungu akipenda), na ataonyesha njia kwa wasafiri.

Adui anapaswa kujua kwamba Upinzani (Muqawamah) dhidi ya unyang'anyi , dhulma, ukandamizaji na kiburi (uistikbari) -yote hayo- hayajaisha (na hayaishi) na yataendelea hadi kufikia mahala panapokusudiwa (hadi kufikia hatima).

Jina zuri na sura angavu ya Syed Hashim Safiyyu al-Din (Radhi za Allah ziwe juu yake) pia ni nyota inayong'aa katika historia ya eneo hili (la kikanda). Alikuwa msaidizi wa karibu (wa Sayyid Hassan Nasrullah) na sehemu muhimu ya Uongozi wa Upinzani (Muqawamah) nchini Lebanon.

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya waja wake wema, na iwe juu ya Mujahidina hawa wawili wennye utukufu, na iwe juu ya wapiganaji (Mujahidina) wengine Mashujaa na wasio na ubinafsi (waliojitoa nafsi zao kwa ajili wa wengine) ambao waliuawa Shahidi hivi karibuni, na pia iwe juu ya Mashahidi wote wa Uislamu. Na salamu zangu za kipekee zikufikieni enyi wanangu wapendwa, vijana jasiri wa Lebanoni.

Sayyid Ali Khamenei

21 - 02 - 2025

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha