Jumanne 6 Mei 2025 - 12:47
Hatua mpya za kuunganisha Hawza na mfumo wa Fedha wa Kiislamu

Kikao maalumu kuhusu Benki ya Kiislamu kimefanyika katika "Jāmi‘at al-Kawthar", Islamabad Pakistan, kikiwa na lengo la kueneza dhana ya kifedha katika uislamu, huku kikihudhuriwa na maulamaa pamoja na wanafunzi wa hawza.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha Tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza, kikao hiki kililenga kueneza mafundisho ya kifedha na kiuchumi yanayozingatia sheria ya Kiislamu, na kilihudhuriwa na wanazuoni, wahadhiri na wanafunzi wa Hawza"*Jāmi‘at al-Kawthar", Islamabad Pakistan.

Katika kongamano hili la kielimu, "Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Shabbīr Ḥasan Maythamī", mjumbe wa Kamati ya Kisheria ya Benki Kuu ya Pakistan, alihudhuria kama mgeni maalumu na kutoa hotuba muhimu.

Kikao hiki kilifanyika kwa muktadha wa mfululizo wa program za kielimu zinazoandaliwa na taasisi ya "al-Ṣādiq", ambazo zinalenga kuongeza uelewa wa wanafunzi na wahadhiri wa hawza kuhusu misingi na miundo ya Benki ya Kiislamu katika nchi nzima. Taasisi hii inalenga kuimarisha uhusiano madhubuti kati ya mafundisho ya dini na mifumo ya kisasa ya kifedha ya Kiislamu kupitia mafunzo ya kitaalamu.

Wazungumzaji katika program hii walieleza nafasi ya benki ua Kiislamu katika jamii ya sasa na umuhimu wa kuikuza. Pia walishirikiana na washiriki mitazamo yao ya kifiqhi, kielimu na kiutendaji.

Kikao hiki kilipokelewa kwa hamasa kubwa na wahadhiri pamoja na wanafunzi. Washiriki, sambamba na kujifunza misingi ya benki ya Kiislamu, walishiriki kwa hali ya juu katika mijadala kwenye kikao. Na hatimaye, baadhi ya washiriki walioteuliwa walitunukiwa zawadi kama ishara ya kuthamini mchango wao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha