Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Kibinadamu, alisema kuwa; uendelevu wa ubinadamu unategemea kuanzishwa kwa mfumo wa haki unaohakikisha haki za wanadamu wote bila ubaguzi, na kuleta haki na usalama kwa kila mtu. Aidha, kudhibiti nafasi ya kidhalimu na kiharibifu ya ubeberu na Uzayuni, ni sharti la msingi la kutimia mshikamano wa kibinadamu katika dunia ya leo.
Katika ujumbe huo, akirejea hali ngumu ya mataifa yaliyodhulumiwa, alisema: leo hii hitaji kubwa zaidi la mshikamano wa kibinadamu ni la watu wa Palestina, hususan wakazi wa Ukanda wa Ghaza; watu ambao kwa upande mmoja wanakabiliwa na dhulma na uvamizi wa utawala wa Kizayuni, na kwa upande mwingine, katika hali ngumu ya baridi ya majira ya baridi, wamenyimwa mahitaji ya msingi kabisa ya kibinadamu.
Aliongeza kuwa: pamoja na Palestina, mataifa ya Lebanon, Syria, Sudan na Rohingya pia yanasubiri kutimia kwa mshikamano wa kweli wa kibinadamu katika ngazi ya kimataifa; mshikamano unaoweza kusimama imara dhidi ya muungano wa vurugu wa ubeberu na Uzayuni, na kuzuia kuendelea kwa uhalifu uliopangwa dhidi ya mataifa.
Ukiukwaji mkubwa wa heshima ya binadamu chini ya kivuli cha ukimya wa dunia
Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Pakistan, huku akikosoa ukimya na udhaifu wa mfumo wa utawala duniani, alibainisha kwamba: ukiukwaji mkubwa na wa wazi zaidi wa mshikamano wa kibinadamu na heshima ya binadamu katika miaka ya hivi karibuni umetokea Ghaza, Lebanon na Syria, lakini kwa masikitiko makubwa, mfumo unaotawala dunia umeshindwa na kubaki bila hatua mbele ya jeuri na uchokozi wa ubeberu na Uzayuni.
Akisisitiza kwamba haki, usawa na amani ni msingi ya mshikamano wa kibinadamu, aliongeza: leo tishio kubwa zaidi dhidi ya mshikamano wa kibinadamu ni mifumo ambayo wanadamu wenyewe wameijenga; mifumo ambayo si tu imeshindwa kulinda haki za binadamu, bali imegeuka kuwa chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama, ubaguzi na dhulma duniani.
Mshikamano, ufunguo wa amani ya kudumu duniani
Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, akirelea historia ya kutangazwa kwa Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Kibinadamu tangu mwaka 2005, alisema: licha ya kupita miaka mingi tangu kutangazwa huko, kwa masikitiko, hata katika karne ya ishirini na moja, dhulma, vita na uvamizi wa karne zilizopita — bali kwa ukali na uharibifu mkubwa zaidi — bado vinaendelea. Kwa mujibu wake, ufunguo wa kufikia amani ya kudumu duniani upo tu katika kutimia kwa mshikamano wa kweli wa kibinadamu; mshikamano unaoweza kueneza usalama kuanzia ngazi ya familia, jamii, serikali hadi mfumo mzima wa dunia.
Alisema: migogoro mingi ya sasa ya wanadamu, ikiwemo ukosefu wa usalama, ukiukwaji wa haki, ukosefu wa usawa, na hata changamoto za kimazingira, ni zao la moja kwa moja la vitendo vya mwanadamu na mifumo isiyofanya kazi na iliyochakaa, ambayo leo ndiyo kikwazo kikubwa zaidi katika njia ya kutimia kwa amani, haki na mshikamano wa kimataifa.
Ukosoaji wa utendaji wa taasisi za kimataifa
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Naqvi, katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alikosoa kwa ukali mwelekeo wa taasisi za kimataifa, akisema: sambamba na kuanza kwa karne ya ishirini na moja, ahadi kama kuanzishwa kwa Mfuko wa Dunia wa Mshikamano na hatua nyingine za kusaidia zilitolewa, lakini karne hiyo hiyo ilishuhudia mashambulizi makubwa ya mabomu Afghanistan na Iraq, kuongezeka kwa migogoro katika Mashariki ya Kati, Burma (Myanmar) na maeneo
Akirejelea uhalifu mkubwa uliotendwa Ghaza, Beirut na Damascus, alisisitiza kwamba: watoto na wanawake katika maeneo haya wamekuwa waathirika wa vitendo ambavyo mifano yake ni vigumu kupatikana katika historia ya kisasa. Kwa hiyo, kutaja siku maalumu au kuandaa sherehe za ishara pekee hakutoshi kujibu mateso ya wanadamu, bali Umoja wa Mataifa unapaswa kwa umakini kamili kuhakikisha utekelezaji wa vipengele vya Mkataba wake na maazimio yake.
Mwisho, alisisitiza kwamba: kutimia kwa mshikamano wa kweli wa kibinadamu kunahitaji jamii ya kimataifa kusimama imara dhidi ya nafasi ya kidhalimu ya ubeberu na Uzayuni, na kuondoa kikwazo hiki kikubwa katika njia ya haki, amani na heshima ya binadamu.
Maoni yako