Jumatatu 22 Desemba 2025 - 20:36
Uwepo wa Mwanazuoni Mashuhuri Duniani Katika Chuo Kikuu cha Baqir al-Ulum (a.s.)

Hawza/ Chuo Kikuu cha Baqir al-Ulum (a.s.) kilimpokea Profesa Farid Esack, mwanazuoni mashuhuri duniani na profesa wa Chuo Kikuu cha Harvard.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Chuo Kikuu cha Baqir al-Ulum (a.s.), kilicho chini ya Ofisi ya Tablighi za Kiislamu ya Hawza ya Kielimu ya Qom, kikiendeleza mwelekeo wake hai wa kupanua maingiliano ya kielimu ya kimataifa, kilimpokea Profesa Farid Esack, mwanazuoni mashuhuri wa Uislamu, profesa wa Chuo Kikuu cha Harvard na miongoni mwa Waislamu 500 wenye ushawishi mkubwa duniani. Katika mfululizo wa vikao vya kielimu, kitamaduni na vya majadiliano, alikutana na wahadhiri, wanafunzi na viongozi wa chuo hicho, na akazungumzia teolojia ya ukombozi, haki na mazungumzo ya dini mbalimbali.

Kikao cha pamoja cha kielimu cha wahadhiri na wanafunzi wa kimataifa

Katika programu ya kwanza, jana kilifanyika kikao cha kielimu kilichomhusisha Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Parsania, Shoja’ Alimirza, Sayyid Hadi Sajjadi pamoja na kundi la wanafunzi kutoka Marekani na Kanada. Kikao hiki kilifanyika katika mazingira ya mazungumzo huru na ya kitaaluma, ambapo washiriki walibadilishana mitazamo na kuuliza maswali yao kuhusu mihimili ya fikra za Kiislamu na tafsiri ya kijamii ya Qur’ani Tukufu.

Kikao na Rais wa Chuo na Naibu wa Masuala ya Kimataifa; majadiliano kuhusu ushirikiano wa kielimu wa kuvuka mipaka

Katika hatua iliyofuata, Profesa Esack alikutana na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Rafi‘i Alawi, Rais wa Chuo Kikuu, pamoja na Sajjadi, Naibu wa Masuala ya Kimataifa, na wakafanya mazungumzo. Kiini cha mazungumzo hayo kilikuwa ni kuchunguza njia za kupanua ushirikiano wa kielimu katika sekta za tafiti za Kiislamu na sayansi ya binadamu, pamoja na kuimarisha maingiliano ya vyuo vikuu katika ngazi ya kimataifa.

Kikao cha wajumbe wa baraza la wahadhiri; kubadilishana hoja katika masuala ya utafiti wa Uislamu

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Chuo Kikuu cha Harvard baadaye alihudhuria kikao maalumu cha kielimu cha wajumbe wa baraza la wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Baqir al-Ulum (a.s.), na akaelezea mitazamo yake kuhusu utafiti wa Uislamu, haki, uondoaji wa athari za ukoloni, na uhusiano wa dini na sayansi ya binadamu kisasa.

Vilevile, wajumbe wa baraza la wahadhiri walijadili kwa kina vipengele mbalimbali vya mitazamo hiyo katika mazungumzo ya kitaalamu, yaliyoambatana na mapokezi mazuri ya kielimu na ubadilishanaji wa mawazo wenye kujenga.

Katika sehemu nyingine ya programu, Profesa Farid Esack alishiriki kikao cha wanafunzi wa Masomo ya Palestina. Kikao hiki kilifanyika kwa anuani ya “Palestina; teolojia ya ukombozi na mantiki ya mapambano,” ambapo profesa alieleza mitazamo yake kuhusu teolojia ya ukombozi wa Kiislamu, haki na mazungumzo ya dini mbalimbali, pamoja na uzoefu wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Kikao hiki kilipokelewa kwa mwitikio mpana wa wanafunzi na kikatoa fursa ya mazungumzo ya kina, na ya uchambuzi kuhusu suala la Palestina.

Mazungumzo ya picha kwenye studio ya “Mfumk wa Maisha”

Profesa Esack pia alishiriki katika mazungumzo ya picha katika studio ya “Mtindo wa Maisha” ya Chuo Kikuu cha Baqir al-Ulum (a.s.), ambapo alizungumzia teolojia ya ukombozi, tafsiri ya kijamii ya Qur’ani na changamoto za sasa za ulimwengu wa Kiislamu. Mazungumzo haya yanatarajiwa kuchapishwa hivi karibuni kupitia vyombo vya habari vinavyohusiana na chuo hicho.

Kuinua diplomasia ya kielimu na hadhi ya kimataifa ya chuo

Uwepo wa Profesa Farid Esack katika Chuo Kikuu cha Baqir al-Ulum (a.s.) unaweza kuhesabiwa kuwa ni hatua yenye athari chanya katika kuimarisha diplomasia ya kielimu, kutambulisha uwezo wa kielimu wa Hawza ya Kielimu ya Qom, na kutimiza dira ya chuo hiki kama kinara wa sayansi za binadamu; mwelekeo unaotokana na kaulimbiu yake ya kimkakati: “Hekima kwa ajili ya maisha.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha