Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Bi Greta Thunberg, mwanaharakati wa misaada ya kibinadamu kutoka Sweden, aliiambia Reuters: Ilikuwa imepangwa kwamba nijiunge kama mshiriki katika safari ya meli ya misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wanyonge wa Ghaza. Lakini wakasema kwamba Israel inapanga kuishambulia meli hiyo kwa mabomu.
Baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali pia waliliambia taifa la Israel kwamba: Mabalozi wa Israel lazima waitwe (kuhojiwa rasmi), lazima wawajibishwe, na lazima watoe majibu kwa sababu ya kukiuka sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwazingira watu wa Ghaza na kuishambulia kwa mabomu meli yetu ya kiraia katika maji ya kimataifa.
Tangia tarehe 2 Machi, Israel imekata rasilimali zote kwa watu milioni 2.3 waishio Ghaza, na hata chakula kilichokuwa kimehifadhiwa wakati wa kusitisha mashambulizi mwanzoni mwa mwaka nacho kimekwisha kabisa.
Harakati ya Hamas pia imetoa taarifa kuhusu tukio hili, ikiishutumu Israel kwa "uharamia wa baharini" na "ugaidi wa kiserikali."
Maoni yako