Kulingana na kundi la Tarjama la Shirika la Habari la "Hawza", marasimu ya mazishi ya Shahidi wa Ummah, Syed Hassan Nasrullah, yatafanyika Jumapili, Februari 23, huko Beirut. Marasimu haya ni fursa ya kuhuisha upya ahadi na maadili ya mashahidi na kuonyesha uaminifu wa watu kwa njia ya upinzani (muqawamah).
Hojjat al-Islam wa al-Muslimeen Syed Mohammad Mahdi Nasrullah amesisitiza katika ujumbe wa video kwamba hafla hii ya mazishi sio tu kuwa ni mazishi rahisi, bali pia ni siku ya kutangaza msimamo na kuonyesha upendo kwa mtu ambaye alijitolea maisha yake yote kwa ajili ya watu na maadili yao. Alisema: Jumapili iko karibu na siku hii ni siku ya kuonyesha uaminifu. Yeyote anayehudhuria marasimu (hafla) hii ya mazishi ataonyesha kuwa yeye ni "mtu mwaminifu".
Maoni yako