Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hazrat Ayatollah Jawadi A'mouli alizungumzia juu ya suala la "Dua bora wakati wa Amali bora" kwa kusema: "Dua bora zaidi itakuwa wakati ule wa tendo / amali bora zaidi, na kwa vile mtu yeyote atafanya jambo jema kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, basi huyo atakuwa pia na Dua iliyojibiwa.
Iwapo mtuataswali Swala ya Faradhi, huyo pia dua yake itakuwa ni yenye kujibiwa, na ndio maana wakasema: Usitoke nje ya chumba cha kuswali (Msikitini) mara baada ya kuswali kwa haraka na mapema, usiondoke mahali hapo pa swala mapema, bali kaa usome / uombe dua. Na hii ni kwa sababu Dua yako inakuwa ni yenye kujibiwa baada ya swala ya faradhi.
Darsa la Tafsiri; Suratul Baqarah: Aya ya 225.
Maoni yako