Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Kikao cha kila wiki cha somo la maadili la Ayatollah Javwdi A'mouli kilifanyika leo (Jumatano) katika Msikiti Mkuu wa Qom kwa sura ya kukutana ana kwa ana; na lililohudhuriwa na watu tofauti tofauti, ambalo alieleza na kufafanua Hekima ya 157 na 158 ya Nahj al-Balagha.
Mheshimiwa Ayatollah alisema: Hadhrat Amir al-Mominin (a.s) anasema katika khutba ya 157 ya Nahj al-Balaghah:
«قَدْ بُصِّرْتُمْ إِنْ أَبْصَرْتُمْ، وَ قَدْ هُدِیتُمْ إِنِ اهْتَدَیْتُمْ، وَأُسْمِعْتُمْ إِنِ اسْتَمَعْتُم»
"Tumeeleza misimamo na njia, na kile unachopaswa kukiona, umekiona, kile unachopaswa kukisikia na umekisikia, lakini kukubali hicho na kukielewa hicho, kunategemeana na mapenzi na irada ya mtu binafsi; Katika khutba ya 20 ya Nahj al-Balagha, mada zinazofanana zimetajwa; Kwa maana kwamba jumbe na mwongozo wa Mwenyezi Mungu umesemwa vya kutosha na sasa inategemea na mtu mwenyewe kwamba je analo sikio la kusikiliza ili asikie na kuelewa au la. Kwa hakika, ikiwa kweli watu watazingatia na kuona jumbe, basi kwa hakika wataelewa na kuongozwa (na kuongoka).
Akasema: Katika Hekima ya 158, Hadhrat Amirul Muuminina (a.s) anasema:
«عَاتِبْ أَخَاكَ بِالْإِحْسَانِ إِلَیْهِ، وَ ارْدُدْ شَرَّهُ بِالْإِنْعَامِ عَلَیْهِ»
Kauli ya Hadhrat yenye nuru na mwangaza ni hii kwamba:
Mtu akikusema vibaya, haraka haraka na wewe ukamsema vibaya, hili ni jambo la kimwili, ni suala la kimaumbile, lakini ukizuia uovu (ubaya) wake kwako kwa kumtendea wema, hili litakiwa ni suala la kiasili (Fitrah).
Hadhrat Ayatollah Jawad A'mouli alisema: Mtu anapofanya jambo baya, unapaswa kumtendea kwa wema, uungwana na utu, na badala ya kujibu mambo mabaya kwa mambo mabaya, unapaswa kuzuia mambo mabaya kwa njia ya kumtendea wema na adabu. Ikiwa unatendewa ubaya, wewe jibu kwa wema na ukarimu, kwa sababu tabia hii inategemea Asili (Fitrah) ya Kibinadamu na ina athari nyingi zaidi kuliko kukabiliana kwa kimaumbile (kimwili) na kuvutana.
Kwa kusema na kubainisha kwamba jamii inapaswa kuelimishwa kupitia Asili (Fitrah), alisisitiza: Jamii inapaswa kukamilishwa kwa kupitia Asili (Fitrah), sio kwa Maumbile, na sio kwa kuchukua na kufunga, sio kwa ukosefu wa akhkaq, lakini ni kwa kutoa msamaha (kusamehe), kwa adhama, kwa ukuu, kwa utukufu na wema. Amirul-Mu’minin Ali (amani iwe juu yake), anasema: Kitu cha kwanza cha kufanya wakati wa kushughulika na uovu (ubaya) wa wengine ni kuzuia uovu (ubaya) kwa adabu, kwa wema, kwa uungwana, kwa ukarimu, kwa utu na urafiki.
Hadhrat Ayatollah Jawadi A'mouli alisema: Suluhisho la kwanza la kusahihisha (kurekebisha) ni njia ya Asili (Fitrah) ya Mwanadamu. Ni wakati ule tu ambao njia hizi (za Kifitrah / Kiasili) hazifanyi kazi ndipo hatua zingine kama vile hatua kali zitahitajika zitumike. Jamii inapaswa kuelimishwa kwa Asili (Fitrah); Kuamrisha mema na kukataza maovu kunaweza kuwa na ufanisi zaidi ikiwa kutafanywa kwa usahihi na kwa njia za asili (Fitrah).
Akasema pia kuwa: Hii ni kauli yenye nuru na mwangaza ya Imam Ali (as) ambaye alisema: Ukitaka kuzuia maovu, kuamrisha mema na kukataza maovu / mabaya, kuna njia ya kufanya hivyo; na njia hiyo ni kuzuia maovu / mabaya kwa wema (na ukarimu). Iwapo jamii inataka kujirekebisha (na kujisahihisha), lazima itumie njia za asili (Fitrah) na sio njia za Maumbile (ya kimwili).
Hazrat Ayatullah Javadi Amoli ameongeza kuwa: Katika Qur'ani Tukufu na Nahj al-Balagha, kuna amri za kurekebisha jamii kwa kuzingatia maumbile ya mwanadamu, ambayo lazima yatekelezwe katika tabia za kijamii na kimaadili.
Katika sehemu nyingine ya Mkutano huu, Hadhrat Ayatollah Jawad A'mouli amesisitiza juu ya ulazima wa kujijua / kujifahamu na kuzingatia Fitrah (Asili ya Mwanadamu) katika Ibada na Mawasiliano na kuwa na mafungamano / mahusiano na Mwenyezi Mungu; na akaongeza kuwa:
Mwanadamu anapaswa kuanzisha uhusiano mahsusi na Mwenyezi Mungu katika Sala na Ibada zake ili kuweza kujiendeleza na kujikuza kiroho.
Ameashiria juu ya umuhimu wa kutembea katika njia ya Asili / Fitrah ya Mwanadamu na akaashiria juu ya athari chanya za Miezi Mitukufu katika njia hii akisema: Wanaadamu wote wanalazimika kuwa na Miezi na miaka maalum na kumwelekea Mwenyezi Mungu kwa kuimarisha ibada zao katika Miezi hiyo.
Mwezi wa Sha'aban ni fursa ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kuimarisha uhusiano wa kiroho kwa Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s). Mwezi wa Sha'ban utumike kwa faida ya kuweza kuufika Mwezi wa Ramadhani na kwa njia hii, katika hali ya kuelewa uhakika wa ibada na kuimarisha uhusiano wetu kwa Mwenyezi Mungu, tutaweza kuifikia daraja ya juu zaidi katika safari ya kiroho.
Maoni yako