Jumatano 29 Januari 2025 - 16:19
Kuheshimu Haki za majirani ni wajibu

Ayatollah Jawad A'mouli alifafanua: Mwenyezi Mungu Mtukufu amefanya kuwa ni wajibu kuheshimu Haki za majirani na yeyote asiyeheshimu Haki hizi anahusika na kauli hii: "Na wanakata yaliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kuungwa".

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Jawad A'mouli alizungumzia suala la "kutunza hali ya ndugu muumini" katika maandiko na kusema:
 «إنّما المؤمنون إخوة»
"Hakika Waumini ni ndugu" [1].

Na asiyeheshimu / asiyejali heshima ya ndugu Muislamu, basi huyo anajumuishwa chini ya kauli ya "kukata yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu kuungwa"

Imamu Sadiq (rehema na amani ziwe juu yake) anasema: Mtu ambaye amekuwa na urafiki na mwingine kwa muda wa miaka 20, Heshima / Hadhi ya urafiki huu hufikia kiwango cha huruma na ujamaa: “Uswahiba wa miaka 20 ujamaa / udugu", (2); kwa mantiki hiyo, athari za udugu na huruma kwa marafiki hawa wawili zinakuwepo baina yao, hivyo mtu anakuwa hana haki ya kumkasirisha rafiki yake wa miaka ishirini na kuachana naye.

Mawasiliano na majirani yanajumuisha eneo la nyumba 40 na hilo hupelekea kuibuka kwa Haki ya ujirani, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewajibisha kuheshimu Haki za majirani, na asiyeheshimu Haki hizi anakuwa chini ya kauli hii: "Na wanakata yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kuungwa." Na bila shaka, upana wa nyumba arobaini sio tu kwa kuzingatia mipaka ya usawa na ya pande nne tu, bali pia inajumuisha majirani / wakazi wote wa maeneo yote ya usawa ya wima (horizontally & vertically). Kwa maana: Wakazi wa upande wa juu na chini pia wanajumuishwa na Wakazi wa pande maarufu.

[1]: Surat Al_Hujurat: Aya ya 10.
[2]: Biharul An'wari: Juzuu ya 71. Ukurasa wa 157.
Tasnim: Juzuu ya 27. Ukurasa wa 561 na 562.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha