Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Taqi Mudarrisi, mmoja wa wanazuoni wa Iraq, alisisitiza hayo wakati wa darsa yake ya kila wiki ya maadili kwa wanafunzi wa Hawza ya mji mtukufu wa Karbala. Alieleza kwamba kujitolea na kujitoa muhanga Bibi Fatimah Zahra (a.s.), pamoja na misimamo yake ya kihistoria, ilikuwa “mfumo halisi wa kinga” uliolinda umma wa Kiislamu dhidi ya kusambaratika na kupotoka.
Aidha, alibainisha kwamba khutba ya milele ya Bibi Fatimah Zahra (s.a.) ndiyo chimbuko la mfumo mpana wa fikra na dini, unaojumuisha falsafa ya ibada, hukumu za Kisheria na malengo yake ya msingi.
Ayatullah Mudarrisi pia alifafanua kwamba kinga na uimara wa jamii hupatikana tu kupitia mshikamano na kuungana makundi ya waumini, makundi ya kijamii na tabaka la wasomi na watu wenye upeo wa kielimu.
Maoni yako