Jumatatu 12 Oktoba 2026 - 15:00
Mmekaa Kimya Miaka 12 Wakati Yemen Ikishambuliwa na Kuzingirwa, Leo Mna Wasiwasi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Riyadh!

Hawza/ Muhammad al-Farah, mjumbe wa Ansarullah ya Yemen, amekosoa ukimya wa baadhi ya nchi mbele ya mashambulizi na mzingiro dhidi ya Yemen kwa kipindi cha miaka 12, akisisitiza kuwa orodha ya malengo ya kijeshi ya Sana’a ni pana na kwamba silaha sahihi pamoja na mbinu za kushtukiza bado hazijaingia vitani.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, mjumbe huyo wa Ansarullah ya Yemen amezungumzia majibu yanayoweza kutolewa siku zijazo na uwezo wa kijeshi wa Sana’a, akijibu misimamo ya baadhi ya watu kuhusu shambulio dhidi ya Uwanja wa Ndege wa Riyadh.

Muhammad al-Farah, mjumbe wa Ansarullah, amekosoa kile alichokiita kujifanya kuonea huruma na kuunga mkono Saudi Arabia kwa baadhi ya watu, licha ya kuielezea nchi hiyo kuwa ni mvamizi mwenye uhalifu ambaye kwa kipindi cha miaka 12 ameharibu viwanja vya ndege vya Yemen. Alisisitiza kuwa orodha ya malengo ya Sana’a ni pana na kwamba silaha sahihi bado hazijaingia katika uwanja wa vita.

Akizungumza na wale wanaolaani shambulio dhidi ya Uwanja wa Ndege wa Riyadh na kuunga mkono upande wa mvamizi, ambaye ni Saudi Arabia, nchi ambayo imeharibu viwanja vyote vya ndege vya Yemen na kuvifunga kwa kipindi cha miaka 12, Muhammad al-Farah alisema: “Tunawaambia: Jiepusheni na lawama zenu, vilio vyenu na machozi ya mamba. Orodha ya malengo ya Yemen ni pana, na silaha sahihi pamoja na mbinu za kushtukiza pia zitaingia katika uwanja wa vita, Mwenyezi Mungu akipenda.”

Alisisitiza kuwa wananchi wa Yemen, ambao wamekuwa wakiuawa na kuishi chini ya mzingiro kwa kipindi cha miaka 12, huku watu hao wakiwa hawajasikia hata tamko moja la kulaani kuhusu yale yanayowakumba wananchi hao, watapata haki zao kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na bila shaka watapata uhuru.

Aliongeza kusema: “Lakini kelele na vilio vyenu havithibitishi kwetu jambo jingine isipokuwa kwamba adui mhalifu, ambaye amewaua watoto wetu na kuharibu nchi yetu, amepata madhara, ameumia na amefikia hali ngumu isiyovumilika. Pia, vinaonesha kuwa mapigo aliyopokea hadi sasa yamekuwa yenye maumivu makali, adui huyu lazima anywe kikombe kilekile alichowanywesha wananchi wetu.”

Chanzo: 26sep.net

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha