Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Gholamhossein Mohseni Ejei, Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alifika katika mojawapo ya hospitali za Tehran na kumtembelea Ayatullah al-Udhma Nuori Hamadani kwa lengo la kumjulia hali yake ya kiafya.
Wakati wa ziara hiyo, mkuu wa timu ya madaktari wanaomhudumia mwanazuoni huyo mkubwa wa kidini aliwasilisha taarifa kuhusu mwenendo wa matibabu yake. Aidha, alieleza matumaini yake kwamba, kutokana na hali yake ya kiafya kuendelea kuimarika, hivi karibuni ataruhusiwa kutoka hospitalini.

Maoni yako