Alhamisi 8 Oktoba 2026 - 08:00
Ubaguzi Unaowalenga Waislamu Wazidi Kuenea Nchini Marekani

Hawza/ Kwa masikitiko, licha ya maeneo yote ya ibada, yakiwemo makanisa na masinagogi ya Wayahudi, kutengewa maeneo ya maegesho katika ramani za miji, bado kuna upinzani mkubwa kutoka kwa mamlaka za manispaa, hususan huko California, dhidi ya kutengewa misikiti maeneo ya maegesho.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, wakati Jumuiya ya Kiislamu ya Santa Barbara ilipofungua msikiti wao mpya uliojengwa mwaka 2019, baada ya kupita takribani miaka 19 tangu waliponunua kiwanja hicho. Kwa masikitiko, miaka 10 kati ya hiyo ilitumika katika mchakato wa kupata vibali kutoka manispaa, mchakato wa ujenzi wa msikiti na upatikanaji wa vibali vyake ulikumbwa na vikao 16 vya kusikiliza maoni ya umma pamoja na vikao vilivyoahirishwa, ambapo wakazi wa mji wa Goleta, akiwemo Waislamu wa eneo hilo, walieleza wasiwasi wao, hususan kuhusu mahali pa kuegesha magari ya waumini, jambo ambalo manispaa haikutoa kibali cha kuanzisha eneo la maegesho kwa ajili hiyo.

Ingawa wasiwasi kuhusu maegesho katika eneo lenye shughuli nyingi unaweza kuonekana kuwa wa kimantiki, watafiti wa usanifu na mipango miji katika Chuo Kikuu cha California, Santa Cruz na UCLA walithibitisha kwamba jumuiya za Waislamu zinazojenga misikiti mipya hukabiliwa kwa kiwango kisicho sawia na upinzani unaojitokeza kupitia tofauti kubwa katika kutengewa maeneo ya maegesho kwenye ramani za miji, na kwamba huu ni ubaguzi dhidi ya Uislamu unaodaiwa kuchochewa na sababu zilizofichika.

Utafiti wao, uliochapishwa katika Jarida la Chama cha Mipango cha Marekani, ambalo ni mojawapo ya majarida yanayoongoza katika uwanja wa mipango miji, unaonesha kwamba uwezekano wa kupingwa ujenzi wa misikiti mipya ni mkubwa kwa asilimia 16 hadi 18 kuliko makanisa mapya yaliyo katika maeneo ya karibu — kiwango ambacho ni kikubwa kwa kiasi kikubwa kuliko kile ambacho kingetokea kwa bahati nasibu.

Mark Fathi Massoud, Profesa wa Masomo ya Kisiasa na Kisheria katika Chuo Kikuu cha California, Santa Cruz, na mwandishi mkuu wa utafiti huo, amesema: “Hofu kuhusu kukua kwa dini na kuongezeka makundi ya kidini yaliyo wachache ipo katika maeneo mengi ya Marekani, licha ya jinsi tunavyothamini uhuru wa kidini. Kuna upungufu wa maeneo ya maegesho kwa Waislamu. Unapoweka dini na maegesho pamoja, unazalisha aina ya ubaguzi uliojengeka ndani ya jamii.”

Chanzo: news.ucsc.edu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha