Alhamisi 8 Oktoba 2026 - 10:00
Sheikh Maher Hamoud Afungua Sanduku la Kumbukumbu za “Sayyid Shahidi wa Umma”

Hawza/ Sheikh Maher Hamoud, Rais wa Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama, alikuwa na uhusiano wa zaidi ya miongo minne na Shahidi huyo mtukufu, ulioanza tangu kukutana kwao kwa mara ya kwanza mwaka 1983, na ambao uliambatana na misimamo thabiti na matukio mengi.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kuna ushahidi na simulizi nyingi zinazoeleza nyanja mbalimbali za shakhsia ya “Sayyid Shahidi wa Umma”, Shahidi mtukufu, Sayyid Hassan Nasrullah. Kila tunapoandika kutoka katika chemchemi ya shakhsia hii ya kipekee na ya kihistoria, ndivyo tunavyozidi kuwa na kiu ya kusikia zaidi. Kila simulizi ni tofauti na nyingine, na kila kisa kinaeleza upande maalumu wa shakhsia ya kiongozi ambaye mfano wake ni nadra katika historia, wakati mwingine tunasikia kisa kimoja mara moja, mbili au hata mara kadhaa, lakini bado tunahitaji kusikia zaidi; kwa sababu tukiwa pamoja na Sayyid, hakuna kuchoshwa na kurudiwa simulizi.

Miongoni mwa watu waliohifadhi kumbukumbu nyingi kumhusu Sayyid Hassan Nasrullah katika fikra zao yupo Sheikh Maher Hamoud, Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama; mtu ambaye alikuwa na uhusiano wa zaidi ya miongo minne na Shahidi huyo mtukufu, uhusiano ulioanza tangu kukutana kwao kwa mara ya kwanza mwaka 1983 na ambao uliambatana na misimamo thabiti pamoja na matukio mengi.

Katika sehemu mpya ya podikasti ya “Al-Ahed”, Sheikh Maher Hamoud anafungua sanduku lake la kumbukumbu na kusimulia kuhusu mkutano wa kwanza, matukio yaliyowaunganisha, misimamo iliyobaki katika kumbukumbu, hadi kufikia maelezo ya kina kuhusu shakhsia ya Sayyid, mahusiano yake na misimamo yake.

Sheikh Hamoud anasimulia jinsi ambavyo katika miaka hiyo ya mwanzo alisema kwamba Sayyid alikuwa na “cheo na hadhi kubwa”, na jinsi alivyomwandikia mwanzoni barua kali, lakini baadaye alishangazwa alipoona hekima yake katika kujibu kwa msingi wa mbinu na mantiki isiyo na mfano. Aidha, anasimulia maelezo ya mkutano waliokuwa nao huko Damascus, pamoja na ndoto ambazo Sayyid alimshirikisha, na pia anafichua maneno yake kuhusu kufariki kwake katika mwezi wa Muharram.

Mbali na hayo, Sheikh anazungumzia maelezo yanayohusiana na akili na undani wa mtazamo wa Sayyid, pamoja na kisa cha mkutano aliokuwa nao na Rafiq al-Hariri, na anaendelea kusimulia hadi kufikia nyakati za mwisho na yale yaliyotokea kabla ya hapo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha