Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Ali Al-Tawil, mchambuzi wa kisiasa, katika mahojiano amesema: Maelekezo ya Marekani na uingiliaji wa Washington ndio sababu kuu ya kuendelea mkwamo wa kisiasa, hususan katika suala la kukamilisha Baraza la Mawaziri.
Al-Tawil amesema: Veto iliyopo kutoka kwa baadhi ya nguvu za kisiasa dhidi ya nguvu na vyama vingine, pamoja na ushindani mkali unaoendelea baina yao, umeleta hali ya mkanganyiko wa kisiasa, ambayo matokeo yake ni kutokamilika uundwaji wa Baraza la Mawaziri na kuendelea kuwa pungufu hadi leo.
Ameongeza: Suala la kutatua hatima ya Baraza la Serikali na kukamilisha nyadhifa zilizobaki katika Baraza la Serikali la Al-Zaydi, halihusiani kabisa na matukio na mvutano unaoendelea katika eneo hili; hususan kwa kuwa eneo hili linakabiliwa na mapambano ya kiuwepo ambayo haiwezekani kutabiri matokeo yake wala muda wa kumalizika kwake.
Amesema kwamba si jambo la kimantiki kulihusisha suala la Baraza la Serikali na matukio ya eneo hili, na kubainisha: “Baraza la Serikali litakamilishwa ima kwa kupata mwanga wa kijani kutoka Marekani, au iwapo kutakuwa na masharti au masuala yanayozingatiwa na Serikali ya Marekani, uamuzi kuhusu hilo utaahirishwa; hususan kwa kuwa kuna maelekezo mengi yanayotolewa na Washington kwa Baghdad.”
Maoni yako