Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Bi. Mulika Laura Enrilo, mwalimu wa hisabati mwenye umri wa miaka 58, alisema kwamba; ingawa baadhi ya wanafunzi wa kike huvaa hijabu, katika kipindi chote cha taaluma yake hajawahi kuwaona wanafunzi wakivaa vazi linalofunika uso shuleni. Alisema huenda katika shule nyingine kukawa na wanafunzi wachache wanaovaa vazi hilo, lakini “hili ni tangazo la kampeni za uchaguzi.”
Aliongeza: “Wanafunzi wa kike nchini Italia ambao wanataka kuvaa hijabu shuleni hufanya hivyo; hakuna anayewasumbua, wala mwalimu wala wanafunzi.”
Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Italia, siku ya Jumapili wakati wa mkutano wa chama chake cha kihafidhina na cha kitaifa kinachoitwa Ndugu wa Italia (FdI), huku akisema kwamba; “mnapaswa kwenda shuleni mkiwa hamjafunika nyuso zenu,” alifafanua marufuku hiyo iliyopendekezwa na kuiwasilisha kama hatua kuelekea usawa wa kijinsia.
Shirika la Habari la Serikali la ANSA limeripoti kwamba kwa sasa ni wanafunzi wa kike kati ya 500 na 600 tu katika nchi nzima wanaovaa mavazi yanayofunika kabisa nyuso zao.
Bi. Laura alisema: “Ikiwa mwanafunzi wa kike atafika shuleni akiwa amevaa vazi linalofunika uso, siwezi kumwambia arudi nyumbani. Wajibu wangu ni kumchukulia kama kijana anayefikiri kwamba anafanya jambo zuri, ninapaswa kumheshimu.”
Yahya Pallavicini, Imam wa Msikiti wa Milan, alisema kwamba; marufuku hiyo imeunda “tatizo la uongo”, na kuelekeza uangalizi wa umma kwenye vazi linalotumiwa na watu wachache sana, jambo ambalo linapotosha “uelewa” kuhusu Uislamu.
Aliendelea kusema: “Hii ni juhudi ya kuwasilisha mfano mmoja wa jamii, ambayo kwa hakika haina uhuru wa mtu binafsi; jamii inayounga mkono ubaguzi wa wazungu, na iwapo kuna jambo lolote tofauti, linatengenezwa kuwa taswira ya kejeli kwa kuitumia siasa na kwa njia ya udanganyifu kweny masuala kama kuvaa vazi linalofunika uso na mengineyo, ili liwe na manufaa kwa siasa.”
Chanzo: Shirika la Habari la Al Jazeera
Maoni yako