Jumanne 17 Novemba 2026 - 08:06
Hawza ya Qum nchini Iran, Yasitisha masomo ya Ngazi ya Juu Mpaka Mwisho wa Wiki Hii

Hawza/ Kufuatia kufariki Ayatullah al-Udhma Wahid Khurasani, Hawza ya Qum, imesitisha masomo yote ya ngazi ya juu kuanzia leo hii mpaka mwisho wa wiki hii:

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Taarifa kamili ya kusitishwa masomo ya hawza ya Qum, ni kama ifuatavyo:

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحیمِ

إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَیْهِ رَاجِعُونَ

Kwa masikitiko na huzuni kubwa, tunatoa salamu za rambirambi na pole kufuatia kifo cha mwanazuoni mashuhuri wa Fiqhi kutoka katika madrasa ya Ahlul-Bayt wa Utume na Utakasifu (amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao), Marji' Mkuu wa kidini, Ayatullah al-Udhma Wahid Khurasani (Mwenyezi Mungu autakase na kuutukuza utukufu wake).

Kwa taarifa hii, tunapenda kuwajulisha kuwa kutokana na msiba huu mkubwa usioweza kufidiwa, masomo ya ngazi za juu (Sutuh Aliyah) pamoja na masomo ya Bahthi Khariji katika Hawza ya Qum yatasitishwa kuanzia leo, Jumanne, tarehe 17 Novemba, hadi mwisho wa wiki hii.

Kituo cha Usimamizi wa Hawza ya Qum

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha