Jumapili 30 Agosti 2026 - 14:19
Hizbullah Yaadhimisha Maulid ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) kwa kufanya Mkutano wa Umoja wa Wanazuoni mjini Sidon

Hawza/ Hizbullah imeendesha katika Jengo la Mtukufu Sayyid al-Shuhadaa (as), lililopo katika eneo la Haret Sidon, hafla kwa mnasaba wa Maulid ya Mtume wa Rehema, chini ya kaulimbiu “Umoja wa Kiislamu, Roho ya Kukabiliana na Ubeberu Dunianj.”

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah imeendesha katika Jengo la Mtukufu Sayyid al-Shuhadaa (as), lililopo katika eneo la Haret Sidon, kutokana na mnasaba wa kuzaliwa kwa Mtume wa Rehema, Mtukufu Muhammad (s.a.w.w.), hafla katika mfumo wa mkutano wa kila mwaka wa kuimarisha umoja kwa mnasaba wa Wiki ya Umoja wa Kiislamu. Hafla hiyo iliitwa “Umoja wa Kiislamu, Roho ya Kukabiliana na Ubeberu Duniank,” na ilihudhuriwa na idadi kubwa ya wanazuoni wa dini.

Msimamizi wa Kitengo cha Ulinganiaji na Shughuli za Kiutamaduni cha Hizbullah, Hujaatul-Islam Sayyid Ali Izzuddin Fihs, alitoa hotuba na kusema: “Adui Mzayuni anajaribu kutekeleza mfano wa Ghaza nchini Lebanon; kuanzia milipuko, mashambulizi ya anga, uharibifu na kuwahamisha watu kutoka makazi yao. Lakini ndani ya nchi kuna vita vinavyoendeshwa kwa lengo la kuchafua sura ya (Muqawama), ambavyo Marekani na Israel wako nyuma yake, ili kuubebesha Muqawama gharama ya yale ambayo adui anayafanya, kwa sababu hawathubutu kumwambia Mmarekani: Wewe unaegemea upande mmoja na sisi hatuwezi kuendelea nawe kwa njia ambayo mazungumzo na hali ya kisiasa vinaendeshwa.”

Aliongeza: “Pamoja na yote yaliyotokea na kujitolea kulikofanyika, Muqawama unaendelea kuwa suluhisho pekee la kudhibiti uasi wa adui huyu na kukabiliana na hatua zake.”

Hujaatul-Islam Fihs pia alisisitiza: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni dola yenye nguvu na mamlaka, na itaendelea kuwa mhimili mkuu.”

Sheikh Maher Hammoud, Mwenyekiti wa “Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama Duniani,” alitoa hotuba na kusema: “Jana nilikutana na Mheshimiwa Balozi wa Iran nchini Lebanon, Muhammad Reza Shaybani, na nilimpongeza kwa lile ‘kofi’ alilompiga Waziri wa Nishati, Yusuf Raji, na Balozi wa Marekani, Michel Issa, kupitia kuongezewa muda wake.” Aliongeza: “Wingi wa watu sio ndio unaofanikisha ushindi, bali kinachohitajika ni kuongeza juhudi mara dufu kwa uelewa kamili ili kukabiliana na hatari ya yale yanayotokea.”

Kwa upande wake, Sheikh Ghazi Haninah, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la “Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu,” alisema katika hotuba yake: “Tumepata mafanikio makubwa ambayo kwa miaka 100 tumekuwa tukilia kwa uchungu ili tuyafikie, tuyaone, tuyashuhudie na tuishi pamoja nayo. Tumeishinda Marekani.”

Sheikh Haninah alikumbushia: “Wakati baadhi ya watu walipokuwa wakisikiliza yale ambayo Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei alikuwa akisema kwamba Marekani lazima iondoke katika eneo hili, baadhi yao walifikiri kwamba hiyo ilikuwa ni kaulimbiu tu zinazotolewa, lakini tumeshinda na tumeishinda Marekani.”

Kwa upande mwingine, Sheikh Hussein Qassem, Mwenyekiti wa “Baraza la Wanazuoni wa Palestina,” alisema: “Adui ambaye mwoga hawezi kuwatisha Waislamu bilioni moja.” Wakati huohuo aliuliza: “Muislamu anawezaje kufurahia chakula na kinywaji wakati watu wa Ghaza wanajikunja kwa njaa na kulala kwenye maeneo ya wazi, na watu wa kusini mwa Lebanon wanateseka kutokana na kuongezeka kwa mvutano wa kila siku wa Israel?”

Aidha, katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la “Jukwaa la Uelewa wa Kiislamu,” Sheikh Saeed al-Qassim, na Naibu Mwenyekiti wa “Jumuiya ya Urwatul-Wuthqa,” Sheikh Fadi Madhi, pia nae alihutubia.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha