Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, “Harakati ya Utamaduni wa Kuunga Mkono Muqawama” na “Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini Lebanon” zimeendesha hafla katika Ukumbi wa Tamuz, mjini Baalbek, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) na Wiki ya Umoja wa Kiislamu.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wabunge Melhem al-Hujairi na Yanal Salih; Mufti Maalum wa Jaafari, Sheikh Ahmad Qabalan; Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama Duniani, Sheikh Maher Hammoud; Marwan Malouf na George Malouf; Askofu Charbel Trad; Sayyid Faisal Shukr; Msimamizi wa Kamati ya Maridhiano katika Harakati ya Amal, Ali Karkaba; Msimamizi wa Haram Tukufu ya Maqam ya Sayyida Khawla; Hussein Nasrullah; Msimamizi Mtendaji wa Baalbek katika Chama cha Kitaifa cha Kijamii cha Syria; Hussein al-Hajj Hassan; viongozi kutoka Chama cha Rayat al-Watani; viongozi wa Palestina; viongozi wa dini; shakhsia za kisiasa na kijamii; pamoja na wenyeviti wa vyama vya wafanyakazi, manispaa na machifu wa mitaa.
Hafla hiyo ilifunguliwa na kocha Sami Ramadan, kwa niaba ya “Harakati ya Utamaduni wa Kuunga Mkono Muqawama”. Alisisitiza: “Muqawama, ukiwa pamoja na unyanyasaji unaowakabili watu wa Ghaza ambao wamebeba mizigo ambayo hata milima haiwezi kuivumilia, unadhihirisha umoja wa kibinadamu na kimaadili.”
Sheikh Qabalan: Enzi ya utawala wa Marekani inazikwa katika Mlango wa Hormuz
Hujaatul-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Maalum wa Jaafari, alisema katika hotuba yake: “Mtu yeyote ambaye si mkali katika kukabiliana na madhalimu na madikteta kama ‘Tel Aviv’ na Marekani, hastahili kuwa pamoja na Manabii na Mitume.”
Sheikh Qabalan aliendelea: “Enzi ya utawala wa Marekani siku hizi inazikwa katika Mlango wa Hormuz na chini ya vifusi vya vituo vya kijeshi vya Marekani. Israel leo inapitia nyakati mbaya zaidi katika historia yake, na kila kushindwa kwa Marekani katika eneo kunamaanisha kushindwa milele kwa Israel, msimamo wetu leo uko wazi: sisi tuko pamoja na Mwenyezi Mungu.”
Mufti Maalum wa Jaafari aliiomba serikali kusimama pamoja na maslahi ya mamlaka ya nchi, watu wake na msingi wake wa kitaifa, pamoja na majukumu yake ya kulinda heshima, hadhi na mamlaka ya Lebanon, ambayo yanadhihirika kupitia jeshi na Muqawama.
Alibainisha: “Kama Muqawama usingekuwepo, Lebanon ingebaki kuwa koloni la kitalii la Kizayuni, muqawama, kupitia historia yake iliyojaa mafanikio, umethibitisha kwamba ndio baba wa kweli wa uhuru nchini Lebanon na unapaswa kufundishwa katika shule na vyuo vikuu, wakati katika vitabu vya historia kuandika neno ‘Muqawama’ ni jambo lililokatazwa, na hii ni usaliti kwa damu ya mashahidi.”
Sheikh Qabalan alihitimisha hotuba yake kwa kusisitiza kwamba; “ushirikiano wa kitaifa ni baina ya Uislamu na Ukristo, na Lebanon ni taifa moja, nchi moja na Muqawama mmoja,” na akaongeza: “Historia huungana tunapomshinda adui. Kwa baraka za kujitolea kwa jeshi la Lebanon na Muqawama, hakuna hofu kwa Lebanon.”
Sheikh Hammoud: Utawala wa Kizayuni unaelekea kuangamia
Kwa upande mwingine, Sheikh Maher Hammoud, Mwenyekiti wa Umoja wa Dunia ya Wanazuoni wa Muqawama, alisema: “Jana Balozi wa Marekani alisema: ‘Maadamu silaha za Muqawama zipo, kwa nini Israel ijiondoe?’ Nchini Lebanon kuna watu wanaojaribu kuulaumu Muqawama; wazo wanalotaka kulieneza ni kuufanya Muqawama kuwa ndio wa kulaumiwa.”
Sheikh Hammoud aliuliza: “Je, kile ambacho Israel inakiharibu kusini mwa Lebanon ni vituo vya Hizbullah? Israel inabomoa nyumba, hospitali na shule, na inakiuka sheria na desturi zote za kimataifa.”
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama alisisitiza: “Utawala wa Kizayuni, hata kama utainuka kiasi gani, unaelekea kuangamia, na wao wenyewe hurudia kusema kwamba utawala wao hautadumu zaidi ya miaka 80.”
Sheikh Ghabris: Tuko mstari wa mbele pamoja na Muqawama katika misimamo yote
Kwa upande wake, Hujaatul-Islam Sheikh Hussein Ghabris, Msimamizi wa Mahusiano ya Umma katika Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu, alisema: “Tunasisitiza wazi kwamba tuko pamoja na Muqawama na pamoja na kila mmoja wa wanachama wa Muqawama; tuko pamoja na Muqawama nchini Palestina, Iraq, Iran, Lebanon, Ghaza na Yemen; pamoja na Hashd al-Shaabi, na katika misimamo yote ya mstari wa mbele ya Jamhuri ya Kiislamu, katika njia ya Imam Khomeini na Imam Khamenei.”
Maoni yako