Jumamosi 22 Agosti 2026 - 00:29
Ahadi adhimu ya wananchi kulielekea Jua la Mapinduzi ilikuwa ni kupinga kwa nguvu ubeberu ulimwenguni

Hawza/ Khatiibu wa Swala ya Ijumaa mjini Qom amesema kuwa; Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi alikuwa mfano bora wa utawala wa Kiislamu wa Kiirani katika dunia ya kisasa, akisisitiza: “Maadui walitumia gharama kubwa kwa miaka mingi ili kuvunja uhusiano kati ya umma na Imam, lakini ahadi yenu adhimu ninyi wananchi kwenye Jua la Mapinduzi ilikuwa kupinga kwanguvu ubeberu duniani.”

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi alisema katika khutba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 30 Mordad 1405 (21 Agosti 2026) mjini Qom, iliyofanyika katika Muswalla wa Quds, kwamba: Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi alikuwa zaidi ya cheo cha kisiasa na kidini; kwani si nchini Iran pekee, bali duniani kote alitambuliwa kama Marji wa kidini na kiongozi wa kiroho kwa watu wote wanaopigania uhuru.

Imam wa Ijumaa wa Qom aliendelea kusema: Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi alikuwa mfano bora wa utawala wa Kiislamu katika dunia ya kisasa; kiongozi mwenye hekima ambaye aliweza, kwa busara yake, kuunganisha kwa kina na bila kukatika utambulisho halisi wa Kiislamu na mapenzi ya kitaifa, na kuunganisha kwa namna bora zaidi dhana ya Uislamu na heshima ya kitaifa.

Akirejelea mamilioni ya watu waliouaga na kuusindikiza mwili wa Imam Shahidi, aliongeza kuwa: Barabara za Iran na Iraq zilishuhudia tukio ambalo linaweza kutafsiriwa tu ndani ya mfumo wa imani na ufuasi wa Wilaya. Kusindikizwa na mamilioni  Kiongozi Shahidi wa Umma, zaidi ya kuwa ishara ya taratibu za maombolezo, ulikuwa uwanja wa kudhihirisha ukweli wa msingi na uhusiano usiokatika kati ya umma na Uimamu. Ushiriki huu ulikuwa ishara ya wazi ya msimamo thabiti wa wananchi katika kushikamana na msingi wa Wilayatul Faqih. Ni wananchi ambao, licha ya tofauti zao za lugha na makabila, walisimama katika safu moja ili kuuonesha ulimwengu kwamba umoja katika dunia ya Kiislamu si kauli mbiu, bali ni ukweli unaojidhihirisha katika uwanja wa matendo.

Msimamizi wa Haram Tukufu ya Hazrat Fatima Ma’suma (sa) alisema: Kushiriki katika msafara wa mazishi wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi hakukuwa kulipa deni la heshima tu, bali ilikuwa ni mapambano ya lazima dhidi ya ubeberu duniani. Maadui walitumia gharama kubwa kwa miaka mingi ili kuvunja uhusiano huu, lakini ahadi yenu adhimu ninyi wananchi kuliekea Jua la Mapinduzi ilikuwa “Hapana” yenye nguvu kwa ubeberu wa dunia. Ushiriki huu ulikuwa wajibu wa kidini na ulazima wa kijamii, ili kuwathibitishia madhalimu kwamba warithi wa Harakati ya Imam Khomeini (ra) hawatarudi nyuma kutoka katika njia iliyomwagiliwa damu safi ya viongozi na mashahidi.

Akirejelea kuzaliwa kwa Mtume (saww) na Wiki ya Umoja, alisema: Kuhifadhi umoja na mshikamano baina ya Waislamu katika zama zote kumesisitizwa na Qur’ani Tukufu, riwaya na mwenendo wa Maimamu (as). Kuhifadhi umoja katika mwenendo wa Maimamu (as) imekuwa mkakati, si mbinu ya muda. Katika zama zetu, ambapo maadui wa Uislamu, hususan Wazayuni wenye kiu ya damu wanaotaka kuwaangamiza Waislamu wote, tunapaswa kushikamana kuzunguka mhimili wa Kamba ya Mwenyezi Mungu na, katika zama za Ghaiba, kuzunguka Wilayat Faqih.

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi alisisitiza kuwa: Mazayuni wataizika ndoto yao ya kuuangamiza Uislamu na Waislamu makaburini, na siku moja watu watashuhudia kuangamizwa utawala bandia wa Israel.

Mwakilishi wa Walii Faqih mjini Qom, akitoa salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Imam Hassan al-Askari (as), alisema: Kipindi cha maisha ya Imam Hasan al-Askari (as) kinagawanyika katika vipindi vitatu: Alikaa miaka 13 huko Madina, miaka 10 huko Samarra pamoja na Imam Hadi (as), na kipindi cha tatu ni miaka 6 ya Uimamu wake, miongoni mwa hatua alizochukua katika kipindi hiki ilikuwa ni kuiandaa jamii kwa ajili ya zama za Ghaiba ya Imam wa Zama (aj).

Imam wa Ijumaa wa Qom, akirejelea kuanza kwa Uimamu wa Imam wa Zama (aj), alisema: Imam wa Zama (aj) daima yuko katika juhudi na jihadi kwa ajili ya kuurekebisha Umma. Kwa sababu hiyo, kusubiri Faraja pia kunapaswa kuwa kwa aina ya tendo lenye uhai, linaloendelea na lenye ari.

Alisisitiza kuwa: Kusubiri kwa kweli hakuwezekani bila ya kuomba msaada kutoka kwa Walii wa Zama (aj). Msaada huo, kwa maana pana, una nguzo nne: Tawassul, Ta’assi, Tawaasi na Tajhiz. Nguzo hizi nne za kuomba msaada na kusubiri Faraja hubadilisha hali kutoka nguvu iliyofichika kuelekea utekelezaji, kutoka dhana ya kinadharia kuelekea uhalisia, na kutoka hali ya kutotenda kuelekea utendaji, na kuwabadilisha wanaosubiri kuwa wasaidizi wenye ufanisi wa Serikali ya Mahdi.

Sifa muhimu za wasimamizi wa misikiti kwa mujibu wa Qur’ani

Ayatullah Saidii katika khutba ya kwanza, akieleza kwamba; kumcha Mwenyezi Mungu kuna athari na baraka nyingi, alisema: Mwenyezi Mungu katika aya ya 29 ya Suratul Anfal ametaja athari tatu za uchamungu na amesema:

«یَا أَیُّهَا الَّذِینَ آمَنُوا إِنْ تَتَّقُوا اللَّهَ یَجْعَلْ لَکُمْ فُرْقَانًا وَیُکَفِّرْ عَنْکُمْ سَیِّئَاتِکُمْ وَیَغْفِرْ لَکُمْ ۗ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِیمِ»

“Enyi mlioamini! Ikiwa mtamcha Mwenyezi Mungu [katika mambo yenu yote], Atakujaeni kwa [uwezo na busara maalumu ya] kutofautisha haki na batili, na Atayafuta madhambi yenu na Atakusameheni; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa.”

Khatiibu wa Swala ya Ijumaa ya Qom, huku akirejelea Siku ya Kimataifa ya Msikiti, alisema: Msikiti ndio taasisi pekee ambayo tangu mwanzo iliundwa na Mwenye kuweka Sheria mwenyewe, na watu wamehimizwa kuilinda na kuitunza. Msikiti ni taasisi takatifu ambayo ndani yake hupangwa kila jambo ambalo Serikali ya Kiislamu inalihitaji, kiasi kwamba wakati wa uhai wa Mtume (saww), ulikuwa makao makuu ya Serikali ya Kiislamu.

Hukumu mbili, ya kuzuia na ya kuamuru, kuhusu usimamizi wa msikiti

Akirejelea kwamba Mwenye kuweka Sheria ametoa hukumu mbili kuhusu usimamizi na uingiliaji wa watu katika msikiti, alisisitiza: Hukumu ya kwanza ni ya kuzuia, ambayo Mwenyezi Mungu ameieleza katika aya ya 17 ya Suratut Tawbah:

«مَا کَانَ لِلْمُشْرِکِینَ أَنْ یَعْمُرُوا مَسَاجِدَ اللَّهِ شَاهِدِینَ عَلَیٰ أَنْفُسِهِمْ بِالْکُفْرِ ۚ أُولَٰئِکَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ وَفِی النَّارِ هُمْ خَالِدُونَ»

“Si haki kwa washirikina kuhuisha misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali wakiwa wanajishuhudisha wenyewe kwa ukafiri [na kuukataa ukweli]. Hao ndio ambao matendo yao yameharibika na yamekuwa bure, nao watadumu motoni.”

Imam wa Ijumaa wa Qom aliongeza: Maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mtakatifu na ametakasika, na nyumba Yake pia inapaswa kuwa safi na takatifu; na mikono ya watu wachafu kisiasa, kiitikadi na kadhalika inapaswa kuzuiwa kuingilia masuala ya msikiti. Kubomolewa kwa Msikiti wa Dhirar, ambao ulianzishwa na washirikina na wanafiki, ilikuwa kwa sababu hiyo.

Akirejelea kwamba hukumu ya pili ni ya kuamuru, aliongeza: Mwenyezi Mungu katika aya ya 18 ya Suratut Tawbah ametaja sifa na masharti matano ya imani ya kweli, kuamini Akhera, kuswali, kutoa zaka na kumcha Mwenyezi Mungu kwa wale wanaosimamia misikiti. Amesema:

«إِنَّمَا یَعْمُرُ مَسَاجِدَ اللَّهِ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْیَوْمِ الْآخِرِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَی الزَّکَاةَ وَلَمْ یَخْشَ إِلَّا اللَّهَ ۖ فَعَسَیٰ أُولَٰئِکَ أَنْ یَکُونُوا مِنَ الْمُهْتَدِینَ»

“Kuimarisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni jukumu la wale tu waliomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wakasimamisha Swala, wakatoa Zaka na wasimuogope yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu; basi, inatarajiwa kwamba hao watakuwa miongoni mwa walioongoka.”

Makundi mawili ambayo daima yamekuwa yakipambana na misikiti

Mwakilishi wa Walii Faqih mjini Qom alisema: Maadui wa Uislamu wanajitahidi ima msikiti usijengwe, au ikiwa utajengwa, usiwe na uhai na usiwe na ufanisi katika masuala ya kijamii na mahitaji ya siku ya jamii. Katika njia hii, makundi mawili yamefanya juhudi kubwa zaidi za kuharibu misikiti. Kundi la kwanza ni Wazayuni, ambao kwa chuki hiyo hiyo waliuchoma moto Msikiti wa Al-Aqsa, ambao ulikuwa Qibla cha kwanza cha Waislamu, na hadi leo wameendelea na uhalifu na uovu wao; huku Waislamu waliodhulumiwa wa Palestina, Yemen, Lebanon na maeneo mengine wakisimama dhidi ya wanaopambana na Waislamu hawa.

Aliendelea kusema: Kundi la pili ambalo, kwa kushirikiana na Mayahudi wanaoupinga Uislamu, linafanya hujuma katika masuala ya msikiti ni wanafiki. Msikiti wa Dhirar pia ulijengwa na wanafiki kwa kushirikiana na washirikina, ili kiwe kituo cha kuharibu msikiti unaoendana na viwango vya Kiislamu.

Akisisitiza kwamba; tunapaswa kuwa waangalifu dhidi ya uingiliaji wa wazi na wa siri wa makundi haya mawili katika ukarabati na usimamizi wa msikiti, alikumbusha: Sote tuna wajibu wa kuifanya misikiti kuwa mahali pa kuwa na ufanisi katika mambo yote ya wananchi. Msikiti ni kioo cha Uislamu na ustaarabu wa Kiislamu, na una nafasi muhimu katika kujenga ustaarabu. Msikiti ni mahali pa kuitana, kuunganisha umoja, kushirikisha nguvu, kujitahidi kutatua matatizo ya wananchi na mfumo wa Kiislamu.

Msimamizi wa Haram Tukufu ya Hadhrat Ma’suma (s), huku akirejelea nafasi ya msikiti katika malezi ya watoto, alisema: Wapiganaji walikuwa wakipelekwa vitani kutoka misikitini; na kwa kufanyika uchaguzi misikitini, hatima ya mfumo iliwekewa msingi ndani ya misikiti.

Akisema kwamba wananchi, kwa kuimarisha na kuhudhuria misikitini, huvuruga mipango mibaya ya maadui, aliendelea: Kwa juhudi za pamoja, tunapaswa kurejesha kazi zote za msikiti ambazo zimesahaulika, kulingana na mahitaji ya wakati, na harakati hii inapaswa kuanzia katika msikiti wa kila mtaa. Njia bora zaidi ya kuusimamia msikiti ni mfano wa Baraza la Wadhamini na Baraza la Utamaduni la mtaa. Baraza la Wadhamini lijikite katika masuala ya miundombinu na vifaa, huku Baraza la Utamaduni, likiwa na Imam wa Msikiti kama mhimili wake, lijikite katika masuala ya kiroho na kijamii ya msikiti, kama vile kuwavutia vijana, kupanga programu za kiutamaduni na kushughulikia matatizo ya kiutamaduni ya eneo.

Alisema: Imam wa Jamaa si kwa ajili ya kuswalisha Swala ya Jamaa pekee, bali anapaswa kuchukuliwa kuwa Imam wa wakazi wote wa eneo hilo. Imam wa Jamaa anapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza jukumu la kimkakati la Kiislamu katika mtaa, na taasisi husika zinapaswa kumfundisha Imam wa Jamaa katika uwanja huu. Mafanikio ya mwisho ya mfumo huu yanategemea kuchaguliwa kwa watu wema wenye moyo wa ushirikiano endelevu na Imam, Baraza la Utamaduni na Baraza la Wadhamini, pamoja na kufuata kikamilifu miongozo ya Kiongozi wa mfumo.

Khatiibu wa Swala ya Ijumaa ya Qom alisema: Ikiwa tuna wasiwasi kuhusu maisha yenye staha na haya katika mtaa na jiji, tunapaswa kufahamu kwamba misikiti ni miongoni mwa nguzo muhimu za kuhifadhi haya na kujisitiri. Ili kuondoa wasiwasi kuhusu masuala kama kuamrisha mema na kukataza maovu, kupungua kwa idadi ya watu, matatizo ya kiutamaduni na kadhalika, tunapaswa kushirikiana kwa umoja na kujitahidi pamoja. Na kama tulivyokusanyika katika medani na kuvuruga mipango ya maadui, tusisubiri taasisi yoyote; bali kwa kutumia nguvu za vijana na watu walio tayari kufanya kazi kwa ajili ya msikiti, tuufanye msikiti wa mtaa uwe hai kwa kiwango kinacholingana na misingi ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha