Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, uwanja wa Haram ya Hadhrat Abul-Fadhl al-Abbas (as) ulishuhudia hafla ya mazishi ya miili ya baadhi ya mashahidi wa Hashd al-Shaabi, ambao waliuawa kishahidi kufuatia hujuma ya hivi karibuni dhidi ya makao ya Hashd al-Shaabi nchini Iraq.
Hafla ya mazishi ilifanyika katika uwanja mtukufu wa Haram hiyo, huku ikihudhuriwa na wahudumu wa Ataba hii tukufu pamoja na kundi la waumini.
Katika hafla hiyo, Swala ya maiti iliswaliwa juu ya miili ya mashahidi hao, na wahudumu wa Haram tukufu ya Hadhrat Qamar Bani Hashim (as) walitekeleza ibada ya ziara. Aidha, walimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awajumuishe mashahidi hao katika rehema Yake pana na azijaalie familia zao subira na ustahimilivu.


Maoni yako