Kwa mujibu wa Kitengo cha Habari za Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Islami Analysis, Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, baada ya kukamilisha ziara yake rasmi ya siku mbili nchini Lebanon, alielezea wasiwasi wake kuhusu kiwango kikubwa cha uharibifu na mateso ya raia, na kutahadharisha juu ya athari za kuendelea kwa operesheni za kijeshi za Israel kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Alisema kuwa yale aliyoyaona kwa macho yake yamemshtua sana.
Türk, katika ziara hiyo, alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Lebanon, Spika wa Bunge, Waziri Mkuu pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu wa nchi hiyo. Aidha, alikutana na wawakilishi wa ujumbe wa kidiplomasia, mashirika ya kiraia na idadi ya watu waliokimbia makazi yao. Kwa kuzingatia mazungumzo hayo na uchunguzi alioufanya akiwa uwanjani, aliwasilisha tathmini ya kina kuhusu hali ya Lebanon.
Uharibifu mkubwa wa maeneo ya raia kusini mwa Lebanon
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, akirejelea matumizi ya silaha za milipuko katika maeneo yenye wakazi wengi pamoja na kuendelea kwa mashambulizi ya anga ya Israel, alisisitiza kuwa; hatua hizo zimesababisha wimbi kubwa la watu kuyahama makazi yao.
Alielezea matokeo muhimu ya Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kama ifuatavyo: Kusambaratika kwa mfumo wa makazi kusini mwa Lebanon, Vikosi vya utawala wa Kizayuni bado vinaendelea kudhibiti maeneo makubwa ya kusini mwa Lebanon, hali hii imesababisha maelfu ya wakazi kuyahama makazi yao na kuwazuia kurejea katika nyumba zao.
Uharibifu mkubwa kusini mwa Mto Litani: Kwa mujibu wa ripoti za uchunguzi wa uwanjani na ushuhuda wa wakazi, vijiji vingi vilivyopo kusini mwa Mto Litani vimeharibiwa kabisa na kwa sasa havifai tena kwa makazi ya binadamu.
Wasiwasi kuhusu mustakabali wa UNIFIL: Türk alionya kwamba kumalizika kwa ujumbe wa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) kunaweza kuhatarisha kwa kiwango kikubwa usalama wa raia, na akasisitiza kwamba suala hilo linapaswa kuzingatiwa katika mipango yoyote ya baadaye kuhusu eneo hilo.
Tahadhari kuhusu uwezekano wa kutendeka kwa uhalifu wa kivita
Türk, akizungumzia kuzuiwa kwa raia kurejea katika makazi yao, alisema kuwa hatua kama hizo zinaweza kuingia katika wigo wa uhalifu wa kimataifa, na akaonya kuhusu hadhi ya kisheria ya operesheni za kijeshi zinazoendelea.
Alisema: "Ofisi yetu, kwa kuzingatia uchunguzi wa kina uliofanywa uwanjani, imerekodi visa vingi vya ukiukwaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Ninasisitiza kwamba baadhi ya visa hivyo, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, vinaweza kwa uwazi kabisa kuhesabiwa kuwa ni uhalifu wa kivita."
Maoni yako