Jumatatu 27 Julai 2026 - 02:30
Kisasi cha damu ya Mazuwari wa Imam Hussein (as) kitakuwa jinamizi la mauti kwa wavamizi

Hawza/ Ofisi ya Muqawama wa Kiislamu ya Kataib Sayyid al-Shuhadaa (as) imeeleza kuwa; kitendo cha kigaidi cha Marekani na utawala wa Kizayuni cha kuwalenga mazuwari wasio na ulinzi wa Haram ya Imam Hussein (as) ni jinai kubwa na ukiukaji wa wazi wa sheria na kanuni za kimataifa.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Ofisi ya Muqawama wa Kiislamu ya Kataib Sayyid al-Shuhadaa (as) katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kupitia taarifa kali, imekielezea kitendo cha kigaidi cha Marekani na utawala wa Kizayuni cha kuwalenga mazuwari wasio na ulinzi wa Haram ya Imam Hussein (as) kuwa ni jinai kubwa na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Aidha imesisitiza kuwa kitendo hicho hakitabaki bila kujibiwa, na walioamuru pamoja na waliokitekeleza watawajibika kwa madhara makubwa yaliyotokana na jinai hiyo.

Matini ya taarifa hiyo ni kama ifuatavyo: Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Taarifa Rasmi ya Ofisi ya Muqawama wa Kiislamu ya Kataib Sayyid al-Shuhadaa (as) ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

«مِنَ الْمُؤْمِنِینَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَیْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَی نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ یَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِیلًا»

Kitendo cha kigaidi, cha woga na cha kihalifu kilichofanywa na muungano wa maovu unaoongozwa na Marekani mhalifu kwa kuwalenga mazuwari wasio na ulinzi na wageni wa Haram ya Imam Hussein (as), kwa mara nyingine kimefunua uhalisia wa kinyama, kiburi na kupinga ubinadamu wa maadui walioapa kuupiga Umma wa Kiislamu.

Janga hili la kutisha na la kinyama ni ukiukaji mkubwa na wa wazi wa sheria zote za kimataifa, mikataba ya haki za binadamu na misingi ya ubinadamu, na bila shaka litakabiliwa na jibu la nguvu, la kuwafanya wajute na adhabu kali.

Ofisi ya Muqawama wa Kiislamu ya Kataib Sayyid al-Shuhadaa ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, inatoa pongezi za shahada na rambirambi kwa tukio la kupaa kishahidi kwa kundi la mazuwari na wapenzi wa Imam Hussein (as), kwa Hadhrat Baqiyyatullah al-A'dham (aj), Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Husseini Khamenei, familia tukufu za mashahidi, taifa adhimu na lenye kusimama imara la Iran, pamoja na watu wote huru na wapenzi wa shule ya Ashura.

Bila shaka, matone matukufu ya damu ya mashahidi hawa watukufu yataendelea kuimarisha mti mwema wa Muqawama na mwendelezo wa njia ya jihadi. Aidha, kuwaadhibu walioamuru, waliotekeleza na waliosababisha jinai hii ni ahadi ya hakika, isiyoweza kukiukwa na iliyo karibu kutimia.

Leo hii, magaidi wavamizi wa Kimarekani, baada ya kushindwa kwa fedheha katika medani za vita, wamevuka mipaka yote ya maadili na sheria za kimataifa na kufikisha kiwango cha juu kabisa cha jeuri na ukatili.

Kuwalenga kwa unyama mazuwari ambao hawana silaha nyingine isipokuwa mapenzi kwa Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein (as), ni ushahidi wa wazi wa kukata tamaa, hofu na kushindwa kimuundo adui mbele ya uwezo wa ustaarabu wa utamaduni wa Ashura na hamasa isiyo na mfano ya Arubaini ya Imam Hussein (as).

Maadui dhaifu na walioghurika kwa ndoto zao wanafikiri kwamba kwa kumwaga damu safi ya washiriki wa matembezi ya Arubaini wanaweza kupunguza utukufu, ukubwa na ushawishi wa mkusanyiko huu wa kimataifa unaovuka mipaka ya mataifa. Hata hivyo, huu ni udanganyifu usio na msingi na uliokusudiwa kutoweka.

Damu safi ya wapiganiaji hawa katika njia ya Mwenyezi Mungu haitapunguza hata chembe ukubwa wa njia hii yenye nuru, bali itaongeza zaidi mshikamano, nguvu na uimara wa Safu ya Muqawama wa Kiislamu katika kung'oa uvimbe wa saratani wa Uzayuni na kuwafukuza wavamizi wa Marekani kutoka katika eneo hili.

Mwishoni, tunatangaza tena kwa msimamo thabiti kwamba jinai za kupangwa na zinazoendelea kufanywa na Marekani dhidi ya raia wasio na hatia na mazuwari wa Imam Hussein hazitabaki bila majibu.

Viongozi wa ubeberu wa kimataifa pamoja na vibaraka wao wa kikanda wanapaswa kusubiri matokeo makubwa, makali na yasiyoepukika ya vitendo vyao vya kigaidi.

«وَسَیَعْلَمُ الَّذِینَ ظَلَمُوا أَیَّ مُنْقَلَبٍ یَنْقَلِبُونَ»

Ofisi ya Muqawama wa Kiislamu ya Kataib Sayyid al-Shuhadaa (as) ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha