Ijumaa 3 Julai 2026 - 05:00
Ratiba Kamili ya Mazishi ya Imam Shahidi Jijini Qom Iran, Yatangazwa

Hawza/ Mwenyekiti wa Kamati ya Kuandaa Hafla ya Kuaga na Kusindikiza Mwili wa Imam Shahidi katika mji wa Qom Iran, amesema kuwa hafla ya kusindikiza mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu itaanzia Haram Tukufu ya Bibi wa Karama kuelekea Msikiti Mtukufu wa Jamkaran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Brigedia Jenerali Fathullah Jamiri, Mwenyekiti wa Kamati ya Kuandaa Hafla ya Kuaga na Kusindikiza Mwili wa Imam Shahidi mjini Qom, alisema katika mazungumzo yake na waandishi wa habari kwamba; mkoa wa Qom umejiandaa kikamilifu kwa ajili ya kuwapokea washiriki wa hafla ya kusindikiza mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Alisema kuwa; Qom, kutokana na nafasi yake ya kipekee ya kidini, kitamaduni na kimataifa, daima imekuwa kitovu cha kuangaliwa na ulimwengu wa Kiislamu, na nafasi hiyo imeongeza wajibu wa viongozi na wananchi wa mji huo kuhakikisha kuwa hafla hii ya kihistoria inafanyika kwa utukufu mkubwa zaidi.

Aliongeza kuwa; tangu siku za mwanzo za maandalizi ya hafla hiyo, kamati mbalimbali za kitaalamu zimeundwa katika sekta tofauti, na idara zote zinazohusika na utekelezaji, uokoaji, huduma, malazi, afya, lishe, usaidizi wa vifaa, usafiri pamoja na usimamizi wa msongamano wa magari zinafanya kazi kwa uratibu kamili ili kuwezesha watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi kushiriki kwa wingi.

Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi cha Imam Ali ibn Abi Talib (as) katika mkoa wa Qom alielezea nafasi maalumu ya Qom katika mtazamo wa mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu, akisema kuwa: Imam Khomeini (ra) mara nyingi alisisitiza kuwa mashahidi wa wanazuoni wa dini wana uhusiano maalumu na Qom. Mtazamo huo, alisema, umeongeza uzito wa jukumu la wananchi na viongozi wa mji huo katika kuupokea mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi.

Aliendelea kusema kwamba, baada ya kuchunguza maeneo mbalimbali yaliyopendekezwa, Barabara ya Mtume Mtukufu (saww) ilichaguliwa kuwa sehemu bora zaidi ya kuswali Swala ya Mazishi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupokea watu, urahisi wa kufikika na uwepo wa miundombinu ya Msikiti Mtukufu wa Jamkaran.

Brigedia Jenerali Jamiri alisema kuwa; muda rasmi wa kuanza kwa hafla utategemea wakati ambao mwili mtukufu utawasili kutoka Tehran. Alifafanua kuwa mipango yote imewekwa kwa msingi wa kuanza hafla hiyo katika saa za mwanzo za alfajiri ili watu wasikumbwe sana na joto la mchana.

Ratiba Kamili ya Mazishi ya Imam Shahidi Jijini Qom Iran, Yatangazwa

Aliongeza kuwa; kama ilivyotokea katika baadhi ya hafla za kitaifa zilizopita, ikiwemo mazishi ya Mashahidi wa Huduma na mashahidi wa Muqawama, huenda muda wa kuwasili mwili ukabadilisha ratiba ya mwisho, na endapo hali hiyo itatokea wananchi watajulishwa kwa wakati.

Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi cha Imam Ali ibn Abi Talib (as) mjini Qom alisisitiza kuwa; Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na familia yake tukufu daima wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa kulinda afya na usalama wa wananchi wakati wa hafla mbalimbali. Kwa msingi huo, mipango yote ya hafla hii imeandaliwa kwa kuzingatia usalama na afya ya waombolezaji.

Alisema kuwa; juhudi zote zitafanyika ili kuwepo mazingira yatakayowawezesha wananchi kushiriki kwa utulivu na utaratibu bila kutokea msongamano au tukio lolote litakalohatarisha afya na usalama wa raia.

Brigedia Jenerali Jamiri aliwataka wananchi kuzingatia maelekezo ya usalama, akisema kuwa; kubeba mabegi makubwa mgongoni na vitu visivyo vya lazima kutawaletea usumbufu wao wenyewe na pia kutasababisha ugumu katika usimamizi wa umati wa watu, kwa hiyo aliwashauri wananchi waepuke kubeba vitu vya aina hiyo.

Aidha alisema; ni jambo la wazi kwamba kuingia na aina yoyote ya silaha za moto au silaha baridi, pamoja na vitu vingine vilivyopigwa marufuku kwa sababu za kiusalama, hakutaruhusiwa, na vikosi vya polisi pamoja na vyombo vya usalama vitasimamia kwa makini utekelezaji wa masharti hayo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha