Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, katika mazingira yaliyojaa kumbukumbu za uaminifu na kushikamana na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu, Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tunisia kiliandaa kikao cha fikra chenye anuani “Ustaarabu wa Kiislamu katika fikra za Imam Khomeini na Imam Khamenei.”
Kikao hiki kilifanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka thelathini na saba ya kufariki mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Ruhullah al-Musawi al-Khomeini, na pia kwa ajili ya kuenzi njia ya Shahidi Imam Sayyid Ali Khamenei, katika mkutano uliokusanya “fikra za kihistoria na uchambuzi wa kisiasa wa kisasa.”
Kikao hicho kilifunguliwa na Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tunisia, Dkt. Jaafar Morvarid. Huku akiwakaribisha wahudhuriaji kutoka miongoni mwa maprofesa wa vyuo vikuu na wanafikra, alisisitiza kwamba roho ya ustaarabu wa Kiislamu imejengwa juu ya misingi miwili muhimu: utambulisho na hamasa.
Dkt. Morvarid alifafanua kwamba “utambulisho” ndio kitu kinachochora mwelekeo wa ustaarabu na kujibu maswali yake ya msingi, huku “hamasa” ikiupa mwelekeo huo maudhui, roho na ladha.
Aliongeza kwamba; hamasa ndiyo njia ambayo Muislamu wa kisasa anaitumia kutafsiri uwepo wake na chaguo lake katika maisha, na akaashiria kuwa mtazamo wa maisha wa Muislamu mwenye kujitolea ni mtazamo wa kihamasa ambao huutazama ulimwengu, mwanadamu na maisha katika mfumo wa uzuri, maana na malengo.
Pia alisisitiza kwamba; changamoto na matatizo ambayo Umma unakabiliana nayo si mambo ya kuvumiliwa tu, bali ni umuhimu wa kuisafisha roho ya mwanadamu; kama vile jiwe la thamani linavyopigwa na kusuguliwa kwenye miamba migumu ya mto hadi likawa johari ya thamani.
Dkt. Morvarid alisisitiza kwamba; mwanadamu Muislamu, kwa baraka ya ufahamu huu, ana uwezo wa kipekee wa kupambana na shari na kuvuka aina mbalimbali za mashinikizo yanayojaribu kuondoa uhuru wa maamuzi yake.
Kwa upande mwingine, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tunisia, Mir Masoud Hosseinian, alisisitiza kwamba; Imam Khomeini hakuwa tu kiongozi wa kisiasa, bali alikuwa mrekebishaji ambaye alijenga katika Umma imani ya “sisi tunaweza.”
Balozi huyo alieleza kwamba; kuambatana kwa kumbukumbu hii na Sikukuu kubwa ya Ghadir kuna maana za kina, kwa sababu Imam Khomeini alikuwa mfano halisi wa mwendelezo wa njia ya Wilayah katika kusimamisha haki na kupambana na ubeberu.
Pia alimwelezea Imam Sayyid Ali Khamenei kama “Imam Shahidi” na kusisitiza kwamba; kwa kipindi cha miongo tisa amekuwa ngome imara dhidi ya njama mbalimbali.
Hosseinian alisisitiza kwamba; mhimili wa Muqawama leo una nguvu zaidi kuliko wakati wowote mwingine, na alieleza kwamba jambo hilo limetokana na mwamko wa mataifa uliochochewa na fikra za Maimamu hawa wawili na miongozo ya uongozi wenye hekima; mwamko ambao umefanya mipango yote ya kuhalalisha uhusiano na utawala wa Israel na kueneza mifarakano kushindwa, na kusisitiza kwamba mapambano yataendelea hadi kuikomboa Quds Tukufu.
Baadaye, mtafiti wa historia Muhammad al-Rassafi al-Miqdad aliwasilisha uchambuzi wa kina kuhusu nadharia ya Wilayat al-Faqih na uhusiano wake na ustaarabu wa Kiislamu, na akayataja Mapinduzi ya Iran katika chimbuko lake kuwa ni “ya Hussein”; mapinduzi yaliyochochewa na misingi ya Imam Hussein (a.s) katika kupambana na dhulma.
Katika mazungumzo maalumu na tovuti ya habari ya Al-Ahd, alisisitiza kwamba Wilayat al-Faqih ni fikra ya kielimu na iliyo wazi, na ni jambo la msingi kwa uongozi wa Umma wa Kiislamu katika zama za ghaiba. Aliongeza kwamba Wilayah hiyo haijafungika tu katika upande wa kawaida wa kifiqhi, bali pia inahitaji uwezo wa kisiasa na uwezo wa kiutawala.
Aidha, Miqdad anaamini kwamba; mafanikio ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran, licha ya vikwazo na vita, ni ushahidi wa kwamba; mfumo huu ni “akiba ya Mwenyezi Mungu” kwa ajili ya kuokoa ubinadamu na kuweka msingi wa ustaarabu mpya ambao utatekeleza usalama na uadilifu chini ya uongozi wenye hekima.
Maoni yako