Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon katika taarifa yake umeelezea matokeo ya mazungumzo ya moja kwa moja yaliyofanyika kati ya utawala wa Lebanon na adui Mzayuni chini ya usimamizi wa Shetani Mkuu, yaani Marekani, kuwa ni ya kukatisha tamaa.
Mkusanyiko huo, sambamba na kukosoa kauli za hivi karibuni za Rais Jenerali Joseph Aoun na Waziri Mkuu Nawaf Salam, umebainisha kwamba: Iran inaweza kufikia makubaliano na Marekani bila kubeba mzigo wa Lebanon; lakini Iran ilisimamisha mara mbili vitisho vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Beirut, na mara ya pili mpaka ilitishia kujiondoa katika mazungumzo. Hata hivyo, inatuhumiwa kwamba inaitumia Lebanon kwa maslahi yake yenyewe, ilhali ukweli ni kwamba hali ni kinyume chake.
Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu ulisisitiza kwamba; Sheikh Naim Qassem ndiye Katibu Mkuu wa Hizbullah ambaye wawakilishi wake katika Bunge la Lebanon walipata kiwango cha juu zaidi cha kura za upendeleo; kwa hiyo yeye pamoja na washirika wa Hizbullah kwa hakika ndio wawakilishi wa matakwa ya wananchi wa Lebanon, ilhali Rais na Waziri Mkuu hawajapima kiwango cha uungwaji mkono wa wananchi kwao.
Mkusanyiko huo unaamini kwamba misimamo iliyotangazwa na Rais na Waziri Mkuu haiwakilishi matakwa ya wananchi wa Lebanon, na ukionyesha kwamba; tafiti za maoni zimethibitisha kuwa wananchi wengi wa Lebanon wanauunga mkono muqawama, uliitaja misimamo yao kuwa “imekataliwa kabisa.”
Taarifa hiyo pia ilieleza kwamba; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni msaidizi mkuu na mtetezi wa Lebanon, na kwamba imekuwa ikitekeleza jukumu hilo kwa uaminifu na kwa sababu hiyo imevumilia matatizo makubwa. Ni Iran hiyo hiyo iliyouunga mkono muqawama hadi kupatikana kwa ukombozi [wa Kusini] mwaka 2000, na kupitia hilo ukombozi wa tatu utapatikana mwaka 2026, ingawa wale waliojiuza kwa Marekani na Israel wanapuuza jambo hilo.
Mkusanyiko huo mwishoni ulitangaza kuunga mkono muqawama na kusisitiza kwamba; muqawama pamoja na Katibu Mkuu wake ni wawakilishi wa matakwa ya wananchi huru wa Lebanon, na ukaongeza: “Tunasimama pamoja nao katika misimamo ya kudumu na yenye heshima ya muqawama hadi ushindi utakapopatikana.”
Maoni yako