Alhamisi 4 Juni 2026 - 23:50
Waziri Mkuu wa Iraq atangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Ayatullah al-Udhma Fayyadh

Hawza/ Ali Al-Zaidi, kufuatia kifo cha Ayatullah al-Udhma Sheikh Muhammad Is’haq Fayyadh, ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa nchini Iraq.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Waziri Mkuu wa Iraq, Ali Al-Zaidi, kufuatia kifo cha Marji' mkubwa wa kidini, Ayatullah al-Udhma Sheikh Muhammad Is’haq Fayyadh, ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa nchini Iraq.

Al-Zaidi katika taarifa yake alisema:

“Tunampa pole Ayatullah Sistani, wananchi watukufu wa Iraq, pamoja na Waislamu wote duniani kote kufuatia kufariki kwa Marji' mkubwa wa kidini, Ayatullah al-Udhma Sheikh Muhammad Is’haq Fayyadh.”

Aliongeza kwa kusema: “Kwa msiba huu wenye maumivu makubwa, sekta ya mijadala ya kielimu, ijtihad na elimu za Kiislamu imepoteza mmoja wa watu mashuhuri wa elimu ya fiqhi; Marji' ambaye ameacha athari na nafasi ya wazi katika kiwango cha fikra na ufundishaji, na pia katika hadhi ya juu ya Hawza ya Najaf Ashraf kwa msingi wa mwenendo wa madrasah ya Ahlul-Bayt wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww), vilevile hatua zake katika kuyakurubisha makundi yote ya Waislamu na kuunga mkono masuala ya haki ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu haziwezi kusahaulika.”

Al-Zaidi mwishoni alisema: “Kwa mnasaba huu wa huzuni, tunatangaza maombolezo ya kitaifa nchini kwa muda wa siku tatu, na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu marehemu huyu mkubwa kwa rehema na radhi Zake pana, aijaalie familia yake na wapenzi wake subira na utulivu.

إنا لله وإنا إليه راجعون

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika Kwake Yeye tutarejea.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha