Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maafisa wa Bahrain wameendelea na uhalifu wao na kutekeleza mfululizo wa ukamataji dhidi ya baadhi ya raia baada ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano ya uchunguzi, kufuatia vita ambavyo vyombo vya usalama vimevianzisha dhidi ya raia wa Kishia nchini Bahrain.
Ukamataji huu uliwahusisha «Nasser Al-Kashri», msomaji wa maombolezo ya Ahlul-Bayt (as), «Hajj Abdul-Jabbar Mirza», «Hajj Hussein Darwish», «Ihab Al-Hamdi», «Ahmad Hassan», «Sayyid Abdullah Majid», «Hussein Al-Khayyat», «Mahmoud Muslim», «Hajj Mahdi Salih», ndugu wawili walioitwa «Ali na Hassan Al-Ghanim», «Ridha Ibrahim Muhammad Hamadah», «Sayyid Hussein Jaafar» na «Muhammad Sarhan».
Maafisa hao hawakuishia hapo tu, bali walichukua hatua ya kuwakamata watoto wawili ambao ni; «Mustafa Yusuf» na «Zain Muhammad Ibrahim».
Katika vijiji vinavyokaliwa na Mashia, hali ya tahadhari ya kiusalama ilionekana, kwa namna ambayo maafisa walipeleka vikosi vyao katika maeneo yanayozunguka vijiji vingi kabla ya kuwakamata baadhi ya raia baada ya kuitwa kwa ajili ya kuwahoji.
Ukamataji huu unafanyika katika mfumo wa kampeni inayozidi kuongezeka inayoongozwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain kufuatia matukio yanayoendelea katika eneo hilo, yakiwemo matukio ya kulengwa moja moja Mashia.
Maoni yako