Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ammar Hakim, kiongozi wa vikosi vya Muungano wa “Dola ya Kitaifa” ya Iraq, siku ya Jumatano katika khutba ya Swala ya Idi mjini Baghdad, alitangaza kuiunga mkono serikali ya sasa ya Iraq inayoongozwa na Waziri Mkuu Ali al-Zaidi, na akataka kuwepo kwa mipango ya kiuchumi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za kifedha zinazoikabili nchi.
Hakim alisema: Eneo letu na dunia vinashuhudia mabadiliko ya haraka ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama, na Iraq leo inakabiliwa na majukumu makubwa pamoja na fursa muhimu, nchi inahitaji juhudi za pamoja, kuunganisha nguvu mbalimbali, kuimarisha uthabiti wa kisiasa, wa kiuchumi na amani ya kijamii kwa ajili ya kujenga mustakabali salama na wenye utulivu zaidi.
Aliongeza kuwa: Baada ya kupewa kura ya imani serikali ya Al-Zaidi na matarajio yaliyopo katika siku zijazo ya kukamilisha baraza la mawaziri la serikali hiyo pamoja na kuidhinishwa kwa watu wanaokubalika na wanaostahili, tunasisitiza kuyaunga mkono kikamilifu mambo yote yatakayochangia mafanikio ya serikali katika kufikia malengo yake.
Ammar Hakim pia alieleza kuwa; serikali ya Al-Zaidi tangu siku ya kwanza imekuwa na jukumu la kuimarisha mambo chanya katika faili lake muhimu zaidi, yaani faili la uchumi, ameeleza mara kadhaa kuwa suala hili linapaswa kuwa miongoni mwa vipaumbele vikuu vya serikali, na akasema kuwa; changamoto za kiuchumi zinatulazimisha kufikiria kuhusu mtazamo tofauti, wenye ujasiri zaidi na wenye uhalisia zaidi.
Aliendelea kusema: Mivutano ya kikanda imeathiri uchumi wa dunia, na Iraq ni sehemu ya mazingira haya, kile kinachohitajika katika hatua ya sasa ni kuimarisha mipango ya kiuchumi na kuhakikisha kuwepo kwa mbadala wa kimkakati ambao utasaidia katika kipindi hiki.
Hakim alisisitiza pia umuhimu wa kutafuta zana za msaada wa kiuchumi na kifedha zilizo na unyumbufu mkubwa zaidi pamoja na kuimarisha uwezo wa serikali wa kuulinda uchumi wa taifa dhidi ya mishtuko na mabadiliko ya ghafla, aidha aliongeza kuwa; kulinda uchumi hakujafungwa tena katika matumizi ya njia za jadi pekee, bali kunahitaji kwenda sambamba na maendeleo ya kidijitali na teknolojia.
Maoni yako