Alhamisi 28 Mei 2026 - 13:00
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Watembelea Kituo cha Utamaduni cha Iran Kilichopo Dar es Salaam

Hawza/ Kituo cha Utamaduni cha Iran kilichopo nchini Tanzania kimepokea ugeni maalumu wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar waliowasili katika kituo hicho kwa lengo la kuendeleza mahusiano ya karibu kati ya taasisi hiyo ya elimu ya juu na Kituo cha Utamaduni cha Iran, ziara hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kielimu, kitamaduni na kijamii kati ya pande hizo mbili.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ujio wa wanafunzi hao uliambatana na mapokezi ya kirafiki yaliyoonesha dhamira ya dhati ya kuendeleza maelewano na kubadilishana uzoefu wa kielimu pamoja na tamaduni za mataifa mbalimbali, ziara hiyo pia ilitoa nafasi kwa wanafunzi hao kujifunza kwa karibu shughuli zinazofanywa na Kituo cha Utamaduni cha Iran katika kukuza elimu na mshikamano wa kimataifa.

Katika ziara hiyo, viongozi na wanafunzi hao walipata fursa adhimu ya kutembelea maonesho ya Shiraz yaliyokuwa yakionesha historia, ustaarabu na urithi mkubwa wa kitamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, maonesho hayo yaliwavutia wageni wengi kutokana na ubunifu wake pamoja na namna yalivyobeba ujumbe wa kirafiki na maelewano kati ya wananchi wa Iran na Tanzania.

Aidha, washiriki wa ziara hiyo walijifunza historia ya uhusiano wa karibu uliodumu kwa miaka mingi kati ya Iran na Zanzibar, uhusiano ambao umeendelea kuimarishwa kupitia elimu, utamaduni, biashara na mawasiliano ya watu wa mataifa hayo mawili, wanafunzi hao walielezwa namna ushirikiano huo ulivyochangia kukuza maelewano na kuheshimiana kati ya jamii hizo mbili.

Kituo cha Utamaduni cha Iran kimeendelea kuwa daraja muhimu la kuwakutanisha vijana, wasomi na wadau wa masuala ya elimu kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania kwa lengo la kujenga mazingira bora ya kubadilishana maarifa na uzoefu, kupitia programu mbalimbali za elimu na utamaduni, kituo hicho kimekuwa kikitoa mchango mkubwa katika kuimarisha urafiki wa kihistoria kati ya Iran na Tanzania.

Wanafunzi waliopata nafasi ya kushiriki katika ziara hiyo walielezea kufurahishwa kwao na namna walivyopokelewa pamoja na elimu waliyoipata kuhusu historia ya Iran, tamaduni zake na mchango wake katika maendeleo ya elimu na ustaarabu wa dunia, baadhi yao walisisitiza kuwa; ziara hiyo imewapa hamasa ya kujifunza zaidi kuhusu tamaduni tofauti na umuhimu wa mshikamano wa kimataifa.

Kwa upande mwwngine, uongozi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran ulisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za elimu nchini Tanzania ili kujenga kizazi chenye uelewa mpana kuhusu tamaduni, historia na maadili ya jamii tofauti duniani, pia ulieleza kuwa; milango ya kituo hicho itaendelea kuwa wazi kwa wanafunzi na watafiti wanaotaka kuongeza maarifa yao katika nyanja mbalimbali.

Ziara hiyo imeonekana kuwa hatua nyingine muhimu katika kuimarisha diplomasia ya utamaduni na elimu kati ya Iran na Zanzibar, huku ikifungua ukurasa mpya wa ushirikiano wenye manufaa kwa vijana na taasisi za kielimu za pande zote mbili, wachambuzi wa masuala ya elimu wanaamini kuwa; ziara za aina hii zina mchango mkubwa katika kujenga urafiki wa kudumu, kukuza maelewano ya kimataifa na kuimarisha mshikamano wa kijamii miongoni mwa vijana.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Watembelea Kituo cha Utamaduni cha Iran Kilichopo Dar es Salaam

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Watembelea Kituo cha Utamaduni cha Iran Kilichopo Dar es Salaam

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Watembelea Kituo cha Utamaduni cha Iran Kilichopo Dar es Salaam

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Watembelea Kituo cha Utamaduni cha Iran Kilichopo Dar es Salaam

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Watembelea Kituo cha Utamaduni cha Iran Kilichopo Dar es Salaam

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha