Jumatano 27 Mei 2026 - 11:30
Hizbullah Yaadhimisha kwa Sherehe Kubwa Kumbukumbu ya “Sikukuu ya Muqawama na Ukombozi” katika Mkoa wa Jabal Lebanon

Hawza/ Hizbullah ya Lebanon kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 26 ya “Sikukuu ya Muqawama na Ukombozi”, iliandaa hafla kubwa katika eneo la Majma‘ al-Bihar lililoko Sablin, katika mkoa wa Jabal Lebanon.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah iliadhimisha kumbukumbu ya miaka ya 26 ya “Sikukuu ya Muqawama na Ukombozi” kwa kuandaa hafla kubwa katika eneo la Majma‘ al-Bihar huko Sablin katika mkoa wa Jabal Lebanon.

Katika hafla hiyo walihudhuria watu mbalimbali mashuhuri, miongoni mwao Mahmoud Qomati, waziri wa zamani na mwanachama wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah; Sheikh Maher Hammoud, rais wa Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama; Tariq al-Khatib, waziri wa zamani; Luteni Jenerali Ali al-Hajj, mkurugenzi mkuu wa zamani wa Vikosi vya Usalama wa Ndani; pamoja na wawakilishi wa vyama vya kisiasa vya Lebanon, makundi na harakati za Palestina, wanazuoni wa dini, watu wa nyanja za utamaduni na jamii, mameya, viongozi waliochaguliwa, familia za mashahidi na umati mkubwa wa wananchi.

Sherehe hiyo ilianza kwa kutoa heshima kwa wimbo wa taifa wa Lebanon na wimbo rasmi wa Hizbullah.

Baadaye, Sheikh Maher Hammoud alitoa hotuba, na kufuatia hilo Mahmoud Qomati alihutubia hadhira akisisitiza kwamba; Sikukuu ya Muqawama na Ukombozi si kumbukumbu ya kihistoria tu, bali ni dhihirisho la njia endelevu ya kusimama imara na kudumu katika misimamo, hasa katika mazingira ya vitisho na mashambulizi yanayoendelea ambayo Lebanon na eneo zima vinakabiliana nayo.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa maonyesho ya kisanii na nyimbo za kizalendo zilizowasilishwa na Hassan Harb pamoja na kikundi chake cha waimbaji, programu hizo zilipokelewa kwa shangwe na ushiriki mkubwa wa waliohudhuria, na ziliakisi kwa uwazi ari ya Muqawama na uzalendo kwa nchi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha